Ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu  kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles KIMEI ameanza utekelezaji wa ahadi zake kwa kasi kubwa.

Siku ya leo amekabidhi kiasi cha shilingi milioni nne ambayo ni ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni kuunga mkono ujenzi wa mabweni ya wasichana kwa shule ya sekondari Ghona kata ya Kahe Mashariki.

"Nawahakikishia ahadi tulizozitoa wakati wa kampeni pamoja na zilizopo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa kushirikiana na serikali, wadau wa maendeleo pamoja na ninyi wananchi tutazitekeleza. Katika kuwathibitishia hilo leo nimefika kukabidhi shilingi milioni nne ambayo niliahidi wakati wa kampeni kuwaunga mkono ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule hii. Nitaendelea kushirikiana nanyi kwa kuendelea kuchangia na kutafuta wadau wengine pia watuunge mkono ili tufanikishe ujenzi huu kwa haraka na kuwapa mabinti zetu mazingira mazuri ya kusoma. Nawaomba ushirikiano ili tuijenge Vunjo yetu kwa kasi." Alisema Dkt Kimei

Katika hafla hii walihudhuria Diwani wa kata hiyo Mhe Kulwa Kamili Mmbando, wajumbe wa bodi ya shule, walimu, wenyeviti wa vijiji kata ya Kahe Mashariki na wajumbe wa kamati ya siasa CCM kata ya Kahe Mashariki.

Share To:

Post A Comment: