NA MWANDISHI WETU, BAGAMOYO.


KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa (MSS) Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Ishengoma amewataka wahitimu wa mafunzo ya Sanaa na Utamaduni kufikiria kujiajiri zaidi ya kuajiriwa.


Akizungumza katika Maafali ya 31 yalifanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt. Ishengoma amesema:


 "Nimefurahishwa sana na risala mliyoisoma mkizungumzia suala la ukosefu wa ajira. 


Lakini cha zaidi ni kwamba kazi za sanaa na utamaduni zina manufaa makubwa kwa mtu aliyejiajiri kuliko kuajiriwa kwani wasanii wengi duniani wameweza kutengeneza fedha nyingi kwa kupitia fursa mbalimbali za kidigital ikiwemo mitamdao ya YouTube na kujinufaisha zaidi." Alisema Dkt. Ishengoma.


Aidha, Dkt. Ishengoma amezungumzia mipango mbalimbali ya Serikali katika kuinua sekta ya Sanaa na utamaduni ikiwa ni pamoja na kuanzisha mifuko mbalimbali na mikopo nafuu ili kuwawezesha wasanii kupata mitaji ya biashara zao za Sanaa na kuweza kujiajiri na sio kusubiri kuajiriwa.


Naye mkuu wa Chuo hicho Dkt. Herbert Makoye amewapongeza wahitimu hao wapatao 134 wa ngazi ya Astashahada na Stashahada na kuwataka kuw Mabalozi wazuri wa TaSUBa.


Dkt Makoye pia amezungumzia changamoto mbalimbali zinazokabili Chuo hicho ikiwa ni pamoja na upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na miundo mbinu mbalimbali.


Kwa upande wao wahitimu wametoa shukrani zao kwa uongozi wa Taasisi hiyo kwa mafunzo bora katika kipindi chote cha masoma yao.


Mwisho

Share To:

msumbanews

Post A Comment: