Friday, 16 October 2020

VIONGOZI WA DINI WAANDIKA WARAKA MZITO KWA VIJANA NA WAGOMBEA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 28.


 


Na.Faustine Gimu Galafoni, Dodoma. 
 
 Viongozi wa dini wameandika waraka mzito kwa vijana na wagombea hapa nchini Kwa kutafakari maisha baada ya uchaguzi mkuu na kuacha kuhamasisha vurugu na badala yake wawe mabalozi wa kutunza amani ya Tanzania  .
 
Hayo yamebainishwa Leo Oktoba 16,2020  jijini Dodoma na Askofu wa kanisa la EAGT Ipagala Dodoma   Dkt.Evance Lucas Chande wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema wao Kama viongozi wa dini wamewaasa vijana kuungana kwa pamoja  Katika kulinda amani..
"Sisi kama viongozi wa dini na wadau wa amani Katika taifa tumepata taarifa za uwepo wa vikundi ndani na nje ya nchi ambavyo vinahamasisha vurugu wakati huu wa kampeni na baada ya kampeni kwa lengo la kushinikiza maslahi yao kinyume na demokrasia ya uchaguzi nchini, tunafuatilia taarifa hizi kwa kina ambazo zinasambazwa kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii"amesema.
 
 
Aidha, alifafanua kuwa"Sisi viongozi wa dini tunawaasa vijana kuungana Kwanzaa pamoja bila kujali itikadi za vyama, tukatae kutumiwa na mataifa ya nje, tumkatae mgombea anayehamasisha vurugu zinazoweza kutuondolea amani na maendeleo"amesema.
 
 
Hata hivyo,amehamasisha kwa wanahabari kuandika habari zinazohamasisha Amani kwa lengo la kujenga utaifa.

”Unajua machafuko yakitokea ni ngumu kufanya kazi zenu za habari hivyo ninawaomba  kutanguliza maslahi ya taifa katika kuandika habari za kuhamasisha Amani ”amesema.

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Pentecoste World Mission Ya Mbeya Samson Mwalyego amesema waandishi wa Habari walikuwa na msaada mkubwa katika kuelimisha jamii juu ya ugonjwa wa Corona hivyo ni wajibu wao pia kuhamasisha masuala ya Amani.

“tunaamini waandishi wa habari walichangia kwa kiasi kikubwa katika kutoa elimu juu yaUgonjwa wa CORONA hapa nchini hadi ilipotoweka na sasa imekuwa historia hivyohivyo wanaweza kutoa elimu ya Amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu na taifa linabaki salama “amesema.

Naye katibu wa Baraza la Waislam Tanzania[BAKWATA]Mkoa wa Dodoma Shehe HUSSEIN RAMADHAN amesema mataifa yote yaliyoendelea kiuchumi hawaamini katika vurugu na maandamano hata kama kuna uvunjifu wa haki za binadamu .

”Mnamo Novemba 22,1963 Rais Wa Marekani aitwaye John Kennedy alifyatuliwa risasi kadhaa akiwa akiwa kwenye kampeni za uchaguzi  na kifo chake kuhusishwa na maadui zake   au mataifa hasimu kwa taifa la marekani ,Huyu Kennedy alikuwa Rais wa 35 wa Marekani ambaye alikuwa maarufu sana duniani na hapa tunajifunza kwamba wananchi wa Marekani waliiachia serikali  kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake,bila kuingia mtaani kufanya fujo ,vurugu wala maandamano “amesema.

 Pia amebainisha kuwa ”Tanzania tumekuwa wasuluhishi wa  Amani au  kimbilio la wakimbizi ambao nchi zao zimekuwa na vurugu mfano,Serikali ya Tanzania imepokea maelfu ya wakimbizi kutoka nchini Burundi,Rwanda,DRC CONGO tangu awamu ya kwanza ya Hayati Julius Kambarage Nyerere na pia imehakikisha Amani inapatikana katika nchi mbalimbali duniani kama vile Liberia,Comoro,Darful,DRC Congo, Kenya na Burundi na hatua hii imetupa heshima  hata kwa mataifa makubwa kama Marekani na Uingereza”amebainisha.

No comments:

Post a Comment