Wednesday, 21 October 2020

Mtega kuendelea kunadi sera za CCM
 Na Esther  Macha,Mbarali


MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mbarali kupitia CCM ,Francis Mtega ameendelea na  na ziara zake za kukinadi chama chake  kuelekea uchaguzi  mkuu wa October 28 mwaka huu  pamoja na kuwaomba wananchi wa kata ya Ruiwa kumpa nafasi  ya kuwatumikia katika nafasi  ya ubunge na kuwaeleza  mambo ambayo atawafanyia  endapo watampa nafasi.


Amesema kuwa anafahamu changamoto za kata ya Ruiwa ikiwemo kituo cha afya,umeme,maji pamoja  na ukosefu wa maeneo ya kilimo  na ufugaji  na kwamba akipewa ridhaa  atahakikisha  hayo yote yanafanyiwa kazi kwa kushirikiana na serikali.


“Uwezo huo tunao na ili  haya yote yatekelezwe  chagueni Magufuli na Mtega na Diwani ili muone balaa lake katika utekelezaji wa miradi ya wananchi “alisema Mtega.


Aidha Mtega alisema pia endapo atapewa nafasi atahakikisha anasimamia miradi ya serikali pamoja na kuhakikisha kuwa anatatua changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wananchi wa kata ya Ruiwa na wilaya nzima ya Mbarali .


MWISHO.

No comments:

Post a Comment