Tuesday, 13 October 2020

Mtega amumwagia sifa Rais magufuli kwa wananchi MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbarali kupitia CCM,Francis Mtega amesema kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni kiongozi pekee duniani mwenye maono na miujiza.


Amesema kuwa  Rais Magufuli aliwaunganisha wananchi na Mungu na ugonjwa wa Corona ukaisha na kubaki historia Tanzania katika hili lazima tujivunie ujasiri wa Rais Magufuli.


Mtega amesema hayo jana wakati wa mkutano wa kampeni  wa kunadi sera za chama  hicho kwa wananchi wa wa kijiji cha Runwa kata ya Igurusi.


Aidha Mgombea huyo amesema kuwa hakuna mtu asiyejua kazi kubwa aliyofanya Rais Magufuli mfano tu ujenzi mkubwa wa miradi ya maendeleo na mipango mingine mikubwa.


"Nawaomba wana Runwa mnipe connection ili niweze kuwaunganisha vizuri pamoja na kuwasemea kero zenu pamoja na kuwaletea maendeleo,hii nitatimiza iwapo mtanichagulia Rais Magufuli na Diwani ili tuweze kufanya kazi pamoja"amesema  Mtega.


Mwisho.

No comments:

Post a comment