MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akipokea maoni ya wanawake wanaouza mbogamboga sokoni juu ya namna ya kuwaboreshea mazingira ya kazi
Mama mwenye mtoto ambaye bado ana mnyonyesha akitoa maoni yake kwa Mbunge Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira juu ya uhitaji wa mazingira wezeshi sokoni ambayo ilani ya CCM 2020-2025 imesema
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kulia akimuelewesha mama mjasiriamali juu ya umuhimu wa kupiga kura
Mama mwenye mtoto ambaye anamnyonyesha akisikiliza kwa umakini ilani ya CCM 2020-2025 imesema nini kuhusu wanawake wajasiriamali wadogo masokoni na wenye watoto wadogo
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara 
Neema Lugangira kulia akijadiliana na wanawake wanaouza mboga sokoni juu ya changamoto zao
MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu CCM (NGOs) Tanzania Bara 
Neema Lugangira amefanya ziara katika masoko ya Kashai, Rwamishenye na 
Soko Kuu ili kuweza kujadiliana na wanawake wajasiriamali kwa lengo la 
kuona namna ya kuboresha miundombinu ili waweze kuuza bidhaa zao kwa 
usalama
Wajasiriamali
 ambao amekutana nao ni wanawake wanauza mbogamboga ikiwa ni muendelezo 
wa kampeni zake za kisayansi ili kuweza kuona namna nzuri ya kuweza 
kuboresha miundombinu hiyo na kuwaondolea kero.
Akizungumza
 wakati wa ziara hiyo, Mbunge Mteule Neema alisema suala la usalama 
katika eneo la kuuza mboga mboga sokoni ni jambo muhimu sana kwani 
litapelekea kuhakikisha viini lishe havipotei.
Alisema
 pia sambamba na hilo walijadiliana na wanawake sokoni wenye watoto 
wanaonyonyeshwa ili kuona namna ya kuweka mazingira rafiki ili watoto 
waendelee kupata uhakika wa lishe bora wakati mama zao wakiwa kazini.
Hata
 hivyo wanawake hao wajasiriamali kwenye masoko ya Rwamishenye, Kashai 
na Soko Kuu walielimishwa juu ya sababu za kuipigia kura CCM na walipata
 elimu ya mpiga kura na kusisitizwa Oktoba 28 kujitokeza kwa wingi.
“Lakini
 pia ndugu zangu wajasiriamali tuhakikishe tunampa kura nyingi za 
kishindo Mhe Rais Dkt John Magufuli kwani amefanya kazi kubwa na nzuri 
kwa kuwapa maendeleo watanzania hususan sisi wanawake “Alisema Lugangira






Post A Comment: