October 14, 2020 nakusogeza tena karibu na headlines za kutokea Mkoani Mbeya ambapo leo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CCM Dr. Tulia Ackson ameendelea na ziara zake za kukinadi chama chake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 28, 2020 pamoja na kuwaomba Wananchi kumpa nafasi ya kuwatumikia katika nafasi ya Ubunge ambapo leo ilikuwa ni zamu ya Ituha kata ya Ilomba.  Dr. Tulia amewaeleza Wananchi hao baadhi ya mambo aliyowafanyia pamoja na atakayowafanyia endapo watampa nafasi.


“Nafahamu kabisa hapa Ilomba tunachangamoto nyingi, tukianza na suala la miundombinu barabara nyingi ni mbovu sasa mkitupatia nafasi tutahakikisha hadi hizi barabara za mitaa zinapitika ikiwezekana kwa lami kabisa. Uwezo huo tunao na ili haya yote yatekelezeke chagueni Magufuli na Tulia muone balaa lake”- Dr. Tulia Ackson


“Hapa kwetu Ilomba tunayo changamoto ya umeme, yapo maeneo umeme unakatika katika na mengine bado hayajafikiwa na umeme licha ya kazi kubwa iliyofanywa na Serikali mnafahamu fika kwamba zinahitajika jitihada zaidi za kuwa na Muwakilishi mzuri ambaye ni kiungo na Serikali ili changamoto kama hizi ndogondogo ziweze kutekelezeka na kiungo huyo kwa watu wa Mbeya ni Tulia Ackson pekeee”- Dr. Tulia Ackson


“Mimi Mbunge wenu maarufu kama Mama wa Connection ndio niliyewasaidia kupata umeme hata katika hayo maeneo machache ambayo yanao huo umeme kwasababu mlikuwa mmekosa msemaji, mnayo mifano mingi ya namna nilivyokuwa nikiwasemea Bungeni kuhusu changamoto hizo na Mawaziri halisi walifika hapa kwa ajili ya kuzitatua, sasa niwaulize tu kama nimeyafanya hayo mkiwa hamjanipa nafasi je mkinipa itakuwaje?”- Dr. Tulia Ackson


“Wana-Mbeya hakikisheni safari hii mnachagua Tulia anayetulia Bungeni, Mbunge asiyetulia Bungeni tunasukuma nje, Mbunge anayetoka nje wakati wa kujadili mijadala ya matatizo yetu wana-Mbeya tunasukuma nje, safari hii Mbeya mjini hatudanganyiki tena na tunakwenda na Tulia”-Dr. Tulia Ackson


“Nimezisikia pia hapa changamoto za maji, sasa nimewaomba hapa mumchague Magufuli, Tulia na Madiwani kwasababu upo mradi mkubwa wa maji tunaoutarajia hapa Mbeya mjini mradi  kutoka Kiwila, huo mradi utazalisha maji zaidi ya lita milioni sabini kwa siku na ndio uhitaji wetu hapa Mbeya mjini ambapo kwa sasa maji yanayozalishwa ni lita Milion harobaini ndio maana kuna uhaba. Mradi huo utagharimu zaidi ya Bilion sabini na tano sasa ndugu zangu mkipeleka Mbunge anayekimbia Bungeni imekula kwako”- Dr. Tulia Ackson

Share To:

msumbanews

Post A Comment: