Na Jusline Marco;Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amekanidhi hundi ya milioni 42 kwa vikundi 12 vya wanawake,vijana na wenye ulemavu fedha zitokanazo na mapato ya ndani ya halmashauri ya Meru wilayani humo.

Akikabidhi hundi hiyo Muro amewataka wanakikundi hao kuwa waaminifu katika kurejesha mikopo hiyo ikiwa ni pamoja na kuitumia kwenye malengo yaliyokusudiwa ili waweze kujikwamuwa kiuchumi na kuondokana na umaskini katika familia zao.

Akitoa taarifa ya utoaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Wilaya ya Meru Hamson Mrema amesema kuwa kwa mwaka huo wa fedha jumla ya vikundi vya wanawake,vijana na wenye ulemavu 116 walipatiwa mikopo kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 300 ambapo kati ya vikundi hivyo,vikundi 99 vya wanawake vimepatiwa kiasi cha shilingi milioni 299.

Ameongeza kuwa katika mwaka huo pia vikundi vya vijana vopatavyo 11 vimepatiwa kiasi cha shilingi milioni thelathini na tano na laki tano(35500000)huku vikundi vya watu wenye ulemavu 6 vimepatiwa kiasi cha shilingi milioni kumi na nane.

Ameeleza kuwa kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi milioni 169 ni fedha zitokanazo na makusanyo ya ndani huku zaidi ya shilingi milioni 183 zikiwa ni fedha za mfuko maalum wa mikopo unaojiendesha.

Vilevile amesema kuwa mkopo huo ni sehemu ya fedha za mwaka 2019/2020 ambazo halmashauri ilishindwa kuzitoa kwa wakati muafaka kutokana na kufungwa kwa mfuko wa malipo na TAMISEMI.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wanawake Wilaya ya Meru CCM Bi.Julieth Maturo amewataka wanavikundi hao kuwa na nidhamu ya pesa kwa kuitumia mikopo hiyo jinsi inavyotakiwa huku wakiielekeza kwenye biashara na shughuli za uzalishaji ili kuweza kuzisaidia familia zao na kuepukana na lindi la umaskini.

Bi.Julieth amewaonya wanawake waliopokea mikopo hiyo kutoitumie kinyume na matarajio kwa kuzielekeza fedha hizo katika shughuli za mbesi na kununua nguo.

"Wanawake wengi wamekimbia ndoa zao na nyumba zao kutokana na mikopo wanayoipata kuielekeza kwenye mambo ambayo siyo ya msingi."alisistiza Bi.Julieth

Akizungumza kwa niaba ya wanawake waliopokea mikopo hiyo Bi.Tabu Swalehe Kisale kutoka katika kikundi cha  Nyemo ameshukuru kuwa fedha hizo zitawasaidia katika kuendeleza mradi wao wa ufugaji wa samaki tofauti na hapo awali kabla ya kipata mkopo hali zao zilikuwa duni hivyo kupitia fedha hizo wataenda kuongeza mtaji wao ambapo amwwataka akina mama wengine kuingiza mikopo hiyo katika miradi ya kuzalisha na si vinginevyo.

Naye mmoja wa kundi la vijana aliyejitambulisha kwa jina la Juliana Boniface kutoka kundi la vifue ameishukuru halmashauri kwa kuwapatia mkopo huo kwa ni wanaamini utaweza kuwainua kutoka hatua waliyonayo kwenda kwenye hatua nyingine katika uchumi ambapo amewahimiza vijana wenzake kutafuta na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika halmashauri wanazotoka ili waweze kujikomboa na wimbi la umaskini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: