Wachimbaji wadogo   wa madini nchini wameshauriwa  kutumia Ofisi za Tume ya  Madini zilizopo Mikoani kwa lengo la kupatiwa elimu  ya namna bora ya uchimbaji wa madini ambao utawasaidia kufanya shughuli  za uchimbaji zenye tija.

Hayo yamebainishwa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu wakati alipotembelea banda la Tume ya Madini kwenye maonesho  ya teknolojia na uwezaji kwenye Sekta ya Madini  yanayoendelea Mkoani Geita.


Mhandisi Kumburu amesema  kuwa, kwa sasa Serikali kupitia Tume ya Madini imeendelea kuweka mazingira salama ambayo lengo lake ni kumsaidia mchimbaji mdogo kwenye shughuli zake za kila siku.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: