Saturday, 19 September 2020

NEC YATANGAZA RASMI JIMBO LA CHALINZE MGOMBEA WAKE RIDHIWANI KIKWETE KUPITA BILA KUPINGWA, SASA WAFIKIA 20


NA ANDREW CHALE

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), leo  18 Septemba imetangaza rasmi idadi ya Wabunge waliopita bila kupingwa na kufikia 20 baada ya Majimbo ya Chalinze na Madaba kuongezeka kutoka 18 ya awali.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles katika taarifa yake kwa umma kuhusu rufaa za wagombea Ubunge na Udiwani, wamefanya uamuzi wa rufaa 616 zilizowasilishwa na Wagombea wa Ubunge na Udiwani.

"Hadi kufikia jana 17 Septemba, tumepokea rufaa 616. Kati ya hizo Ubunge 160, Udiwani 456, na malalamiko 25 na rufaa zilizojirudia 44. Alisema Mahera.

Ambapo katika rufaa hizo wagombea waliorejeshwa ni 66 na wagombea ambao hawakurejeshwa ni 32.

"Rufaa zilizokataliwa na kuomba kuenguliwa wagombea 57 na rufaa zilizojirudia ni 5 na kufanya jumla ya yote kuwa 160. Alisema Mahera

Mahera aliongeza kuwa, wamerejesha  wagombea 3 wa majimbo ya Bukene, Kavuu na Namtumbo ambapo sasa yataendelea na uchaguzi kama kawaida.

Aidha, Mahera amesema NEC ilipokea taarifa ya kujitoa kwa Wabunge wa majimbo ya Chalinze na Madaba  na kubaki wagombea pekee waliopita bila kupingwa.

"Kufuatia kumalizika kwa kipindi cha pingamizi na rufaa. Wagombea waliopita bila kupingwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 44 cha tume ya taifa ya uchaguzi sura 343 wagombea ni 20. Tume itawatangaza katika gazeti la Serikali kwa mujibu wa Sheria." Alimalizia Mahera.
Mwisho.

No comments:

Post a comment