Tuesday, 8 September 2020

MGOMBEA URAIS NRA AMPIGIA DEBE MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE


NA MWANDISHI WETU

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Leopard Lucas Mahona, amempigia debe Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ili kumpa kazi kwenye 'Cabinet' yake.

Mahona ameyasmea hayo wakati wa mkutano wake wa kuomba kura za kuchaguliwa nafasi ya Urais kupitia chama chake hicho cha NRA aliofanya leo Chalinze.

Katika mkutano huo, Mahona aliamua kumpigia debe ya moja kwa moja kwa Mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete ambaye tayari NEC imeshamtangaza kupita bila kupingwa jimbo hilo la Chalinze.

"NRA katika kufanya tathimini zetu. Nimeona  mtani wangu Ridhiwani anatosha kuendelea kuwa Mbunge wa jimbo hili.

Na bahati nzuri nimetembea hili jimbo kuanzia mwanzo mpaka mwisho, nimekuja kugundua kwamba jimbo la Chalinze ni kubwa sana." Alisema Leopard Mahona.

Aidha, Leopard Mahona amesema jimbo hilo ni moja ya majimbo makubwa yaliyokaa vibaya kijografia kutoka eneo moja hadi jingine.

"Jimbo la Chalinze endapo utaanzia kule Bagamoyo hadi huku maeneo ya Chalinze  basi utatumia umbali wa kilometa 200'.

Kwa kusema hayo. Niombe
Oktoba 28 muende mkamchague Mbunge, mtoto wenu, kijana wenu Ridhiwani  nimtume kazi ya kwenda kuwasemea na kwenda kupanga mipango ya maendeleo  ya kushirikiana nae kwa sababu mimi  naona anafaa kuwepo hata kwa 'cabinet yangu nitakayoenda kuiunda" Alisema Leopard  Mahona Mgombea Urais wa NRA.

Chama hicho cha NRA hakikuweza kusimamisha wagombea wa nafasi ya Udiwani na Mbunge wa jimbo hilo ambapo hadi sasa upinzani ukibakia kwa Kata Sita huku Kata Tisa zikipita bila kupingwa pamoja na Mbunge mwenyewe wa jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete.

Akizungumza Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alisema , anamshukuru sana Mheshimiwa Mahona kwa kuona juhudi hizo lakini alimkumbusha kuwa ufundi wa utekelezaji huo ni kwa sababu ya ushirikiano aliopewa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na pia Madiwani wa Halmashauri hiyo.  Hivyo yeye aliomba Ndg. Mahona amuunge mkono mgombea wa Urais CCM ili kuleta maendeleo kwa Taifa ilikuendeleza kazi alizoanzisha.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment