Thursday, 17 September 2020

KKKT wazindua mradi wa Afya wa mabadiliko ya mwili katika Shule ya Sekondari Ekenywa


Na,Jusline Marco;Arusha

Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini kupitia Idaya ya Jinsia limezindua mradi wa Afya wa mabadiliko ya mwili kwa kugawa taulo za kike na nguo za ndani kwa wanafunzi wa kike ambao ni wahitaji pamoja na vitabu 6000 vya makuzi kwa vijana wakike ambapo kila jimbo litapokea vitabu 1000 huku vitabu vya mimi mwili wangu na mungu 1500 vitatolewa kwa vijana wa kike na wakiume.

Akizindua  mradi huo Naibu Katibu Mkuu,Misioni na Uinjilisti wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Mch.Jason Kahembe amesema kuwa mradi huo ambao utahusika na kuwasaidia watoto kike kupata vifaa vya kujikinga wakati wa hedhi umelenga kuwafikia watoto wa kike walio vijijini na wenye uhitaji mkubwa.

Aidha mch.Kahembe amewataka wazazi kuhakikisha wanatimiza mahitaji kamili ya watoto wa kike hasa mahitaji ya kibaiolojia kwani kundi hilo ndilo lenye chsngamoto kubwa katila suala zima la ukuaji wa mabadiliko ya mwili ambapo amewasihi akina mama kuwa karibu na watoto wao kwa kujenga mazingira yatakayomfanya mtoto kuwa wazi kuwaeleza mahitaji yao.

Vilevile ameongeza kuwa ukosefu wa mahitaji muhimu kwa mtoto wakike kunapelekea kuwepo kwa ushawishi mkubwa ambao unaweza kumuingiza mtoto huyo na ni chanhamoto kubwa ambayo wazazi wasipowasaidia ni rahisi kwao kujiingiza katika vitendo vya ukahaba ili waweze kutimiza mahitaji yao hivyo kupitia mradi huo ambao umefadhiliwa na wanafunzi wa kanisa la Denish Rutheran Mission lililopo nchini Denimac wataweza kuwafilia wasichana wengi zaidi.

Ameongeza kuwa ili mradi huo uweze kuwa endelevu ni jukumu la lila kanisa kutoa michango yao na kuweza kuwasaidia wasichana wenye changamoto ya vifaa vya kujihifadhi wakati wakiwa katika mzunguko wao wa hedhi.

Akitoa taarifa za utekelezaji wa mradi huo,Katibu wa Idara ya Jinsia kutoka katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Bi.Loikelo Sanga amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuondoa mtazamo hasi uliojengeka kwa jamii kwa kipindi cha vizazi vilivyopita kuhusiana na mabadiliko ya mwili kwa vijana wanapofikia umri wa kupevuka ambapo changamoto kubwa imeonekana kwa mtoto wa kike kwasababu hali hiyo huonekana kama ni uchafu au laana hivyo hupelekea mabinti hao kuona kama wametengwa na pengine kushindwa kabisa kuhudhuria masomo yao.

Ameongeza kuwa kama watekelezaji wa mradi huo wamekuja na mbinu ya kutoa elimu kwa jamii ili kuwasaidia watoto wa kike kujiamini,kuwa huru,kuwa na ujasiri katika vipindi vya hedhi pamoja na kumfanya kuwa chachu ya mabadiliko kwa wengine sambamba na kumuwezesha kufanya kazi zake za kawaida kwasababu wengi wao hukumbana na changamoto nyingi pindi wanapoingia katika mzunguko wao wa hedhi.

Pamoja na hayo Loikelo amesema lengo la kuwahusisha vijana wa kiume katika mradi huo ni ili kuondoa mtazamo hasi ambao jamii wanao hususani jamii ya kifugaji ili wajue kuwa ni mfumo ambao mungu aliuweka kwa wanawake wote.

Ameeleza kuwa kama idara wamajipanga kuwafikia wasichana walio katika maeneo ya vijijini kwa kuziangalia zaidi shule zilizopo katika majimbo 6 ya Dayosisi pamoja na shule za serikali kwa kulenga wasichana wenye uhitaji walio kwenye maeneo yasiyofikika ambayo yana changamoto hizo ambapo mkakati walionao ni kutoa mafunzo kwa wazazi ili kuweza kuondoa mtizamo hasi walionao kusudi kuweza kumfanya mtoto wa kike akaishi kwa amani ndani ya jamii inayomzunguka.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo mwakilishi kutoka Denish Lutheran Mission Bi.Ruth Bach-Svenden amesema kuwa mradi huo ambao unazindiliwa katika majimbo yaliyo chini ya kanisa la KKKT unatokana na michango ya wanafunzi kutoka nchini Denimac kwa kujali na kutambua changamoto zinazowakumba watoto wa kike katika kipindi cha ukuaji.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati Bi.Rose Makara amesema kuwa uzinduzi wa mradi huo katika Shule ya sekondani Ekenywa ni uwakilishi wa shule nyingine ambazo zitafikiwa na utekelezaji wa mradi huo ambapo amewataka watekelezaji wa mradi huo kuepuka laana ya Mungu kwa kuupeleka mradi huo kwa walengwa kwa uaminifu.

"Sisi Dayosisi tunajitahidi kutafuta mbinu zote njema za kuwasaidia ili katila kipindi cha ukuwaji muweze kupita salama na kuwa mfano wa mabadiliko chana katika jamii.'alisisituza katibu mkuu

Sambamba na hayo ameeleza kuwa mafanikio ya mradi huo ni kuweka mafunzo katika vitendo na kubadili mtazamo hasi uliojengwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine juu ya mabadiliko ya miili ambapo amesema kuwa ni matumaini kuwa mradi huo utakuwa na ufanisi mkubwa na kuwafikia walengwa halisi.

No comments:

Post a comment