Saturday, 26 September 2020

HUU NI "USANII" MKUBWA KWA WATANZANIA WAPINZANI KUTAKA KUUNGANA KATIKATI YA KAMPENINa William P. Ndilla

Kama kweli Octoba 3,2020 Vyama vya Upinzani Tanzania yaani Chadema na ACT-Wazalendo watakuja na tamko kwa Watanzania kwamba moja wapo ya Vyama hivyo viwili vimeamua kumuunga Mkono Mgombea Mmoja wapo"Gentleman's Agreement" hii itakuwa kituko Cha Mwaka.

Kuna aina mbili Kubwa za "Party Alliance" duniani kote ambazo ni Pre-Election na Post Election alliance" lakini hakuna "alliance" inayofanyika wakati au katikati ya Kampeni ziliendelea,hii ya Chadema na ACT-Wazalendo  itakuwa ndio ya Kwanza Katika demokrasia ya Africa.

Pre-Election alliance inajengwa kwenye makubaliano ya kutengeneza Umoja Kuelekea Uchaguzi na makubaliano hayo mara nyingi uongozwa na makubaliano ya kisheria na kuamua kuteua Mgombea Mmoja kwa ajili ya Kupambana na "giant" Kama ilivyokuwa UKAWA Mwaka 2015.

Makubaliano ya Pili ya Ushirikiano yaani "Post -Election Alliance" or "Coalition" Ujengwa Katika dhana ya kutafuta Umoja baada ya Matokea ya Uchaguzi hili kuweza kutibu "vidonda" vilivyosababishwa na Uchaguzi.

Lakini pia Post -Election Alliance ujengwa Katika kutafuta Nguvu ya Pamoja Miongoni Mwa Vyama na kuamua Kuanza mapema harakati za kujiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mpya"Next Election".

Ni nadra Sana kuona Vyama vinaingia kwenye Kampeni za Uchaguzi na Ilani na Wagombea wao na katikati ya Mchakato wa Uchaguzi"Kampeni" vinaamua "Kuunga Mkono" Mtia Nia Fulani na ndio Maana Mimi  naiita ni " Gentlemen's
Agreement".yaani Makubaliano ya kishikaji.

Makubaliano Yoyote ya Kisiasa kuelekea Uchaguzi yaani "Party  Alliance" ujengwa na Misingi Mikubwa Mitatu.

Msingi wa Kwanza ni Uhalali wa kisheria na Uhalali huu Upatikana kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa,Sasa Sijui ni kwa kiasi gani Ndugu zangu "WAPINZANI"Wataenda Kutimiza takwa hili kwa Muda huu.

Msingi wa Pili ni "legitimacy" Kutoka Mlengo wa wenye Chama kwa maaana ya Wanachama wa Chadema au ACT-Wazalendo. Makubaliano Yoyote ya kumuunga Mkono Mgombea wa Chama fulani katikati ya Kampeni lazima yapite kwenye Vikao halali vya Vyama husika.

Msingi wa Tatu wa Makubaliano ya Kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ni kutamka wazi wazi kwamba Sisi Chama fulani tunaunga Mkono "Ilani" ya Chama fulani au "Mgombea"wa Chama fulani.

Ni Muhimu Sana Kusema na kutenganisha haya kwa wapiga kura kuwa Makubaliano yetu ni Kuunga Mkono Ilani ya Uchaguzi au Mgombea Kama Mtu na bahati Mbaya sana wakati wa Uchaguzi Chama kinaenda kumuuza Ilani kwa Maana ya "Mkataba" na sio Mgombea.

WATANZANIA TUNAPASWA KUWAULIZA WAPINZANI JE WANAUNGA MKONO ILANI YA CHAMA FULANI AU WANAMUUNGA MKONO MGOMBEA WA CHAMA FULANI?

Kuna Mtego Mkubwa wa Kisiasa hapa ambao Unaweza kukipa heshima Chama kimoja na kukidhofisha Chama kingine.

Swali la Msingi ambalo Watanzania watapaswa wawaulize Chadema au ACT-Wazalendo baada ya Kuunga Mkono Chama kimoja wapo ni Je,WANAUNGA MKONO Ilani ya Chama husika au wanaunga Mkono Mgombea?,

Kama wanaunga Mkono Ilani ya Chama fulani wanataka kuwaambia nini Wanachama wao?Ilani ya Uchaguzi ujengwa kwenye kitu kinaitwa "Ideology" ya Chama hivyo Kuunga Mkono Ilani ni Kuunga Mkono "Ideology"ya Chama fulani.

Kumuunga Mkono Mgombea wa Chama fulani pia sio sahihi Sana Maana Mgombea uongozwa na Ilani"Ideology" ya Chama Chake kwahiyo kwa Vyovyote vile Pana Mashaka Makubwa Sana kuhusu Makubaliano haya.

KWANINI VYAMA HIVI VIMEAMUA KUUNGANA WAKATI HUU?

Sababu ya wazi ya Muungano huu baadhi ya Vyama kukosa fedha kwa ajili ya Kampeni"Kukata Pumzi" hivyo kupelekea kushindwa kuwafikia Watanzania.

Makubaliano haya baina ya Vyama hivi viwili yatakuwa ya "kisaani" Sana kwa Sababu yanatokana na "Njaa" kwenye Vyama vya Upinzani.

MPANGO HUU UNAENDA KUMNUFAISHA NANI?

Lazima Wapinzani waelewe kuwa Mpango wao huo wa "Kitoto" Kama utatokea utaenda kuinufaisha Sana CCM Kuliko Chadema Wala ACT-Wazalendo. Kwanini nasema hivyo?

Wapinzani watakuwa wameonyesha wazi kuwa kwa Wapiga kura kuwa hawana ajenda ya Pamoja Kama Wapinzani hivyo kukosa kuaminika na hii ni kwa Chadema na ACT-Wazalendo.

Pia Kuna Uwezekano Mkubwa kura za ACT-Wazalendo nyingi zitaenda CCM baadala ya kwenda Chadema Kutokana na Wanachama Wengi wa ACT- Wazalendo kutokuhusishwa kwenye Mchakato huo wa Makubaliano ya Kuunga Mkono Chadema.

Kwa Upande wa "Un decided Votes" yaani wapiga kura ambao bado hawajafanya Maamuzi Kuna Uwezekano Mkubwa wa kuipigia kura CCM Kuliko Chadema au ACT -Wazalendo Sababu watakuwa wamekosa Imani Upinzani wote Kama Jumuiya.

MAKUBALIANO HAYA YANAASHIRIA NINI KWA WAPIGA KURA?

Moja ni Kukata tamaa kwa Wapinzani kwamba kuiondoa CCM kwa Nguvu ya Chama kimoja kimoja Cha Upinzani ni sawa na kusukuma treni.

Zitto Kabwe aliwahi kunukuliwa akisema"Itakuwa Ngumu Sana kuiondoa CCM Madarakani kwa Nguvu za Chama kimoja kimoja,Zaidi ya kuunganisha Nguvu" japo Sio tafsiri rasmi.

Mbili ni ishara ya Upinzani kukosa Msimamo,Mikakati ya Pamoja ya Mda Mrefu.
Wapinzani Kama wanajua kuwa kura Milion Sita(6+)walizozipata Mwaka 2015 Chini ya UKAWA ilikuwa ni Sababu ya Muunganiko wao na sio kitu kingine,wanashindwaje kujifunza?

Tafsiri ya Tatu ni kuwa Wapinzani wanakosa Kuaminika kwa Sababu wenyewe wameshindwa kuaminiana na kuweza kuweka Mazingira mazuri ya kusimamisha Mgombea Mmoja na wameamua kufanya "alliance" hii Siku 25 kabla ya Uchaguzi.

HITIMISHO NA NINI KITAENDA KUTOKEA OCTOBA 28,2020?

Ni wazi kuwa Mipango hii ya Zima Moto itaenda kuinufaisha CCM Kuliko Chama kingine Chochote na Sababu ziko wazi.

Kuna Mwandishi Mmoja wa Makala Ole Mushi anasema Kujiondoa kwa ACT-Wazalendo na Kujiondoa kwa Membe kwenye Mbio hizi kutafanya CCM ipoteze kura kwani wapiga kura watahisi Membe alitumwa na CCM.Hapana.

Benard Membe alishafukuzwa na CCM,Benard Membe hakuama CCM Kama walivyofanya Wakina Edward Lowassa kwahiyo kuhusisha Maamuzi ya ACT-Wazalendo "Kukata Pumzi" na kuamua Kujiondoa kwenye Mbio hakuna Mahusiano Yoyote na CCM.

Zaidi CCM inaenda kuchukua kura zote za ACT-Wazalendo Kigoma na Maeneo Mengine na Chadema kuukubali Mpango huu Kwao Una faida na hasara wakae wakijua hilo.

Kura za CCM Mwaka huu 2020 zinaenda kuongezeka Mpaka kufikia Asilimia themanini"80" na kura za Chadema na Upinzani kwa Ujumla zinaenda kupungua Zaidi.

William Peter Ndilla
0759 929244

No comments:

Post a comment