Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza kimezindua rasmi kampeni zake huku Mgombe Ubunge Jimbo hilo Dkt. Angeline Mabula akiwaomba wananchi wamtume tena kwa miaka mingine mitano ili aweze kumalizia kazi na kuibua mambo mengine ya kimaendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo uliofanyika katika uwanja wa Sabasaba kata ya Ilemela, Dkt. Mabula amesema, kwa kipindi cha miaka mitano wamefanikiwa kutatua migogoro ya ardhi, kutoa mikopo ya kinamama, vijana na walemavu kupitia asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri, kujenga na kuboresha miundombinu ikiwemo shule, barabara pamoja na usafiri katika kivuko cha Bezi na Kayenze.

Kulingana na kuboresha miundombinu katika sekta ya uvuvi pale walipokuwa wanakusanya mapato ya Sh. milioni 30 yameongezeka na sasa wanakusanya zaidi ya Sh. milioni 100 ambapo changamoto zilizobaki ni za kupapasa hivyo amewaomba tena wamchague ili akamalizie.

“Wananchi mnamtambua wazi mlipotoka, mlipo lakini mnapoelekea hampajui hivyo mkikiamini Chama cha Mapinduzi na mtambue kina dhamira ya dhati kuhakikisha Taifa linasonga mbele huku mwelekeo wetu ukiwa ni chanya katika kuijenga Tanzania mpya,usiniunue betri mpya ambapo katika betri zako katikati ukaweka guzi hapo tochi haitawaka hivyo nawaomba mnitume ,niwatumikie kwa sababu mie ni kiungo mshambuliaji nitakaye waletea maendeleo,”amesema Dkt. Angeline.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: