Monday, 17 August 2020

VPL MSIMU 2020/21 KUANZA SEPTEMBA 06, RATIBA HII HAPA.


Bodi ya Ligi Kuu imeweka hadharani Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (Vpl) msimu 2020/21 ambayo itaanza rasmi Septemba 06, 2020.

Katika mzunguko wa kwanza Septemba 6-7 mechi tisa (9) zitapigwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini wakati mabigwa watetezi Simba SC wanaanzia mkoani Mbeya kuikabili Ihefu Fc iliyopanda daraja msimu uliopita.

Yanga wao wataanzia nyumbani wakikipiga na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Namungo FC vs Coastal Union uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, Biashara United vs Gwambina uwanja wa  Karume, Mtibwa Sugar vs Ruvu Shootinf uwanja wa CCM Gairo, Dodoma vs Mwadui uwanja wa Jamhuri, KMC vs Mbeya City uwanja wa Uhuru.

Septemba 07, Azam FC vs Polisi Tanzania uwanja wa Azam Complex, Chamazi huku Kagera Sugar wakivaana na JKT Tanzania kwenye uwanja wa Kaitaba.

Mechi ya kwanza ya watani wa jadi Simba vs Yanga itapigwa Jumapili Oktoba 18, 2020 Saa 11:00 jioni katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment