WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa kijiji Langata kabla ya zoezi la kunyoma nyavu haramu

Mkurugenzi mtendaji wa TADB Bw. Japhet Justine akizungumza na wavuvi jana pale ufukweni Tanga

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akichoma nyavu haramu

 

 Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, amewataka wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi katika Bwawa la nyumba ya Mungu Wilayani mwanga Mkoani Kilimanjaro kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano na  kukataa kabisa shughuli za uvuvi haramu.


Mpina ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo aliposhiriki katika kuteketeza kiasi cha makokoro  thelathini na nne (34)yani  nyavu haramu, zilizokamatwa na jeshi la police kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya hiyo katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu katika kijiji cha langata.


“Wizara peke yake haitaweza, Serikali peke yake haitaweza, kila siku tunaambiwa kuhusu uvuvi haramu, nyavu mumenunua kwa gharama kubwa leo zinaenda kuchomwa moto wakati ufike sasa shughuli za uvuvi haramu zikome.” Alisisisza Mpina.


Aliendelea kusema  wapo watu wanafikiria kuwa ikifika wakati wa uchaguzi wataendelea na shughuli hizo na hawata kamatwa, alisema mtu yoyote atakayefanya uvuvi haramu hata siku ya uchaguzi akiwa katika mstari wa kupiga kura atakamatwa na sheria itachukua mkono wake.

 

 “hizi Rasilimali za uvuvi zinatakiwa kulindwa usiku na  mchana, rasilimali hizi ni za kwenu sisi mumetupa jukumu la kzilinda tu, na sisi viongozi wote tutapita tuu ila hzi rasilimali zitabakia kuwa za kwenu” Alisema


Awali akiongea nakusikiliza malalamiko ya wafugaji katika Wilaya ya Same, Waziri Mpina Alisema kuwa wafugaji wataendelea kusikilizwa na kuwataka wataalam wa wizara ya mifugo na uvuvi kupitia team maalum ya kutatua migogoro kushughulikia migogogoro inayowakabili wafugaji katika wilaya za Same, Mwanga na Lushoto.


Waziri Mpina pia aliwataka wakulima na wafugaji kuitumia kwa faida Bank ya Taifa ya Maendeleo ya kilimo katika kupata fursa za kuweza kuchukua mikopo ya riba nafuu ili kuweza kuinua mitaji yao kwa mfano wavuvi kununua na kutumia zana za kisasa za uvuvi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ndugu Japhet Justine, alimuhakikishia Mhe. Waziri kuwa, Bank hiyo ipo tayari kuwawezesha wafugaji na wavuvi kupitia  vyama vya ushirika chini ya usimamizi na udhamini wa wakurugenzi wa Halmashauri husika.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: