Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kufungua mafunzo kwa wakaguzi wa ndani na Watakwimu wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha mapema leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Mchumi na Mtakwimu wa mkoa wa Arusha Mathias Seif akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya Ufunguzi wa Mafunzo funganishi ya uhasibu kwa vituo vya kutolea huduma yanatoendelea kwa siku mbili kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha mapema leo jijini Arusha 
 Sehemu ya wahiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ugunguzi wa mafunzo hayo mapema leo jijini Arusha kama walivyokutwa na kamera ya matukio kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha



Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesisitiza kuwa muongozo wa matumizi ya fedha kuimarisha mifumo ya mahesabu FFARS utasaidia kuweka udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali.

Kwitega ameyasema hayo wakati akifungua semina kwa wakaguzi wa ndani na watakwimu kutoka halmashauri zote za mkoa wa Arusha inayoendelea kwa siku mbili jijini Arusha

Alisema kuwa Tamisemi imetoa muongozo kwa ajili matumizi ya kifedha kwa kutumia mfumo uitwao FAC ili kuimarisha mfumo wa hesabu namna unovyotoa huduma kwenye sekta ya Afya na mashule.

Alisema kuwa wakaguzi wa ndani watakwimu kwenda kufanya ukaguzi wa mifumo hiyo katika halmashauri zote za mkoa kwa kuwa unyeti wa mafunzo hayo na umuhimu wake kwa wakaguzi ni kuweka ulinganifu wa matumizi
sahihi ya mapato na fedha za serikali.

Aidha alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuweka udhibiti kwa halmashauri na mkoa kwenye Takwimu sahihi na wakati muafaka wakati serikali imekuwa inatoa fedha zake matumizi ya fedha na mapato kwa
kutumia mfumo huo kwenye maeneo yote ya serikali.

"Unyeti na umuhimu wa mfumo huu utasaidia kuimarisha mapato na matumizi kwenye halmashauri zetu na mkoa kwa lengo la kuongeza ufanisi na kutoa huduma bora kwa wananchi"

Kwa upande wake Mchumi na Mtakwimu wa mkoa wa Arusha Mathias Seif Alisema kuwa mafunzo hayo ya siku mbili yanawashirikisha wakaguzi wa ndani na watakwimu toka halmashauri saba za mkoa wa Arusha.

Alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha wakaguzi wa ndani kufanya ukaguzi kwenye mifumo ya fedha na Watakwimu kuweza kufanya uchambuzi wa takwimu za fedha zinazopelekwa kwenye vituo vya kutolea
huduma FFARS na kuandaa taarifa kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji na matumizi mbalimbali.

Alibainisha kuwa Takwimu sahihi zinapelekea maamuzi sahihi kwa wakati muafaka jambo ambalo wakati wa utekelezaji kila moja awe na weledi ujuzi wa kutosha kuifanyakazi kwa makini mkubwa kwani serikali ya
awamu ya tano suala hilo ni jambo nyeti sana.

Alisisitiza kuwa kutakuwa na ufuatiliaji karibu wa fedha zinazokuja zinazopokelewa zinazotumika na zinazobakia ili kuwepo kwa mnyororo wa thamani katika matumizi ya fedha za serikali.

Mafunzo ya mfumo funganishi wa uhasibu na utoaji taarifa kwenye vituo vya kutolea huduma FFARS kwa wakaguzi wa ndani na watakwimu utasaidia kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuweka uwazi

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: