Picha ni Kabula Juma Sukwa akiwa kwenye ofisi za UWT mkoa akiwa na Katibu wa mkoa wa umoja huo akipokea fomu za kugombea nafasi ya ubunge wa viti maalum kupitia umoja huo leo jijini Arusha.
Pichani ni Kabula alipowasili kuchukuwa fomu akipata maelekezo na.utaratibu kabla ya kukabidhiwa fomu leo jijini Arusha.
Pichani ni Mfanyabiashara Maarufu Mustafa Panju akipokea fomu ya kugombea nafasi ya ubunge mapema leo jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha


Pichani ni wakili Maarufu Albert Msando akipokea Fomu kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Arusha Denis Mwita leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha


Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wakati wagombea wa nafasi ya ubunge kupitia chama cha mapinduzi wakichukuwa fomu kuomba ridhaa ya chama hicho kupeperusha bendera ikiwa siku ya pili Leo huku wagombea wakifika 69 ndani siku mbili.

Mvuto huo umekolezwa leo baada ya wakili maarufu Albert Msando kuchukuwa fomu kuomba ridhaa ya wanachama kugombea nafasi hiyo kupitia chama hicho ikiwa ni mlolongo wa wagombea akiwemo Philemon Mollel Mrisho Gambo na Kalist Lazaro waliochukuwa jana.

Aidha katika nafasi ya viti maalum kupitia umoja wa wanawake UWT yupo mwanadada maarufu Kabula Juma Sukwa ambaye ameonyesha njia kwa wanawake wengine kuomba ridhaa hadi jioni ya leo zaidi ya kinamama 39 wamejitokeza kuomba nafasi hizo.

Duru za kisiasa mkoani hapa zinaonyesha kuwepo kwa kimuhemuhe na wanachama wanakazi kubwa kuona nani ni nani kujua atapitishwa na chama hicho kuopeperusha bendera kwenye bunge lijalo.

Hata hivyo mchuano utakuwa mkali kwa wagombea kutokana na wingi wao kila moja akionyesha nia ya kutaka kuhudumia wananchi kupitia nafasi za ubunge ndani ya chama hicho kikongwe nchini.


\
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: