Na,Jusline Marco;Arusha

Waziri wa madini Mhe. Dotto Biteko amewataka maafisa madini Mikoa kuwa waadili katika kazi zao huku wakiepuka utoaji wa taarifa zisizo na usahihi kwa umma ili kuwaepusha migongano ya taarifa kwa wananchi.

Biteko ameyasema hayo wakati akizungumza na maafisa madini mikoa katika mkutano wa mwaka wa maafisa madini mikoa wa majumuisho kati ya menejimenti ya wizara na Tume ya Madiji uliofanyika jijini Arusha.

Katika mkutano huo Mhe.Biteko amesema kuwa mwaka wa fedha uliopita wizara ilikadiria kukusanya mapato yatokanayo na madini ya zaidi ya shilingi Bilioni 470 ambapo ilifanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 528 sawa na asilimia 12.3

Aidha amesema ni vyema maafisa madini wakafuata sheria ili kuepuka migogoro kwani wanaishi na jamii ya wafanyabiashara wa madini wanaotaka faida ya haraka hivyo wahakikishe taarifa za uongo au ukweli zinazokuja ofisini kwao wazifanyie kazi bila kumuonea mtu.

"Msinunue migogoro ya watu kwani mkuu wa wilaya amepewa uhalali katika eneo lake la kiutawala na kufanya uamuzi wa kitu ukakosea kidogo lakini haupati uhalali wa weww afisa madini kumkosoa hivyo ni vyema akapeleka malalamiko katika ngazi ya katibu tawala mkoa kwa ajili ya usuluhishi."Alisema Waziri Biteko

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Madini,Prof.Simon Msanjila amemuelekeza katibu mtendaji wa tume na kamishna wa madini wakae pamoja na kupitia namna ya kutekeleza au kutafuta usuluishi wa mapendekezo yao pamoja na kuandaa taarifa itakayoonyesha ni kwa namna gani watayatekeleza ili maafisa madini mikoa waweze kupata taarifa na kusaidia namna ya kutekeleza pale watakapohitajika.

Ameongeza kuwa kufuatia utekeleza mzuri katika sekta ya madini kumepelekea kuongezeka kwa bajeti ya wizara ya mwaka 2020 kwa milioni 11.
"Sasa hivi natembea kifua mbele kwani mlinituma kukusanya bolioni 470 nimekuletea bilioni 528 sasa niongeze nyingine nikakusanye nyingi zaidi na ndiyo maana bajeti ya wizara ya mwaka huu imeongezeka kwa sababu ya mafanikio hayo."alisema Msanjila

Naye  Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof.Idrissa Kikula amesrma moja ya majukumu ya Tume ni kukusanya maduhuli pamoja na kutatua migogoro hivyo yanapaswa kutendewa kazi kwani sekta ya madini inakuwa kwa asilimia 17 hivyo kila mmoja ajiweke sawa kuhakikisha asilimia hizo zinapanda na kufikia asilimia 20 ili kuweza kupandisha hadhi sekta ya madini.

Sambamba na hayo amewahimiza maafisa hao kuendelea kuhakikisha malengo ambayo wamepewa na uongozi wanayatekeleza ili kuweza kilinda hadhi na heshima ya wizara kwa kuwahamasisha wengine kuweza kufanya kazi kwa bidii.

Mwenyekiti wa maafisa madini mikoa Fredi Antoni amesema shughuli za madini zinatekelezwa kwa kufuata sheria na kuzingatia usalama na utunzaji wa mazingira hivyo ameahidi kwa niaba ya maafisa madini watatekeleza maelekezo ya waziri na kufikia lengo hilo lililopangwa la ukusanyaji mapato.
Share To:

Post A Comment: