Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt.John Pima akiongea na Watendaji wa Mitaa na Kata pamoja na wakuu wa idara alipoktana nao kujadili jinsi ya utendaji na kuongeza mapato ya halmashauri hiyo kwenye kikao kazi katika ukumbi wa shule ya msingi Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Sehemu ya watendaji wa Kata na Mitaa wakifuatilia kwa kina maelekezo ya mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.John Pima hayupo pichani kwenye kikao kazi katika shule ya msingi Arusha jana 

Baadhi ya Watendaji wakifuatilia kwa kina kikao kazi na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dkt.John Pima mapema jana katika ukumbi wa shuele ya Arusha School picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt John Pima,amewagiza watendaji wote wa
kata na mtaa wa Jiji hilo kuhakikisha wafanya biashara wadogo wana
vitambulisho vya umachinga na waliyo na vitambulisho wasibugudhiwe
katika biashara zao ila watakaobainika hawana vitambulisho hivyo
kuwafungia kufanyabiashara.

Dkt Pima ametoa maagizo hayo leo alipo kuwa akiongea na watendaji wa
kata na vijiji pamoja na wakuu wa idara katika kikao mkakati cha
utendaji kazi  ili waweze kubadilisha mwenendo wa utendaji kazi zao na
kuwataka watendaji hao kuwa wazalendo katika taifa kwa kufanya kazi
zao kwa weledi wa hali ya juu kwa kusimama katika majukumu yao.

 "Hatuta cheka na mfanya biashara yeyote asiyekuwa na kitambulisho cha
umachinga na akisema hana pesa afunge biashara yake kwanza mpaka
atakapo pata pesa ya kulipia kitambulisho pasipo hivyo hakuna kufanya
biashara na  pia nimepata taarifa baadhi yenu watendaji mnakuwa na
visingizio kwa sababu zenu binafsi wenda mnafanya pia biasha hizo
hizo",Amesema Dkt Pima.

 "Kwa wafanya biashara wote wenye vitambulisho wasibugudhiwe kwa
chochote kile na kuanzia kesho hakuna mtendaji kukaa ofisi wote mwende
kwa wananchi kuhakikisha yeyote anayestahili kuwa na kitambulisho awe
nacho kuepusha changamoto zinazo weza mkuta kwasasa awamu ya tano
inahitaji mtendaji anaye jitambua katika utendaji kazi",Aliongeza Dkt
Pima.

Aidha pia Dkt Pima ameahasa watendaji hao kutoweka visingizio vya
mfumoko wa kisiasa katika jiji la Arusha kwa kutotimiza wajibu wao na
kuwataka wasisjihushishe katika maswala ya siasa badala yake wafanye
kazi zao kwa weledi na kuacha na mambo ambayo hayawahusi katika kazi
zao za kuwatumikia wananchi na kuwataka waelewe muelekeo wa serikali.

Awali Watendaji hao wakitoa changamoto zilizo wafanya kutotimiza
majukumu yao kwa kiwango kikubwa ni baada ya uongozi uliyo kuwepo
kuwaachia zoezi hilo la uuzaji wa vitambulisho wenyewe hali iliyo
pelekea zoezi hilo kuwa gumu pia wananchi kulalamika kutokuwa na fedha
za kulipia vitambulisho hivyo kitu ambacho siyo cha kweli.

 Katika zoezi la utoaji wa vitambulisho kwa wafanya biashara wadogo
hapa Nchini jiji la Arusha lilipewa vitambulishe Elfu hamsi na nane
nazoezi hilo la uuzaji wa vitambulisho hilo kwa wafanya biashara
linatakiwa kukamilika Julai 15 mwaka huu.

 Ameahidi kuwa atawapa ushirikiano katika utendaji wake kwa lengo la
kusaidia kukaza mapato ya halmashauri hiyo na kuendelea kuwaonya
kutambua kwa kina malengo ya serikali ya awamu ya tano kwani mmoja
wenu akitokea hajui malengo hayo atupishe kwani hawezi kwendana na
kasi ya kukuza uchumi wan chi yetu huu sio muda wa mtumishi
kutojitambua ni kufanyakazi kwa mujibu wa viapo vya maadili ya
utumishi wa umma.

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: