MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa ibada maalumu ya maombolezo iliyofanyika wilayani Muheza kwenye viwanja wa Jitegemee na kuongozwa na Mkuu huyo wa wilaya na wananchi wakiwemo viongozi wa dini kwa ajili ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu nchini Benjamini Mkapa



Padre wa Kanisa katoliki wilayani Muheza

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu akizungumza wakati wa ibada hiyo maalumu ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza

Msanii wa mziki wa Dansi nchini Babu Seya akieleza namna Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa alivyowasaidia wasanii


Msaanii wa Mziki wa Bongo Fleva Mwana FA akizungumza

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu akisaini kitabu cha maombolezo kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza

Bendera ikipepea nusu mlingoti

Sehemu ya viongozi wa dini wilayani Muheza ambao wamejitokeza kwenye ibada hiyo

Sehemu ya wananchi wilayani Muheza ambao wamejitokeza kwenye ibada hiyo




WATANZANIA wametakiwa kumuenzi aliyekuwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamini Mkapa kwa yote aliyowaasa katika uhai wake ikiwemo suala la uwazi na ukweli.

Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ibada maalumu ya maombolezo iliyofanyika wilayani Muheza kwenye viwanja wa Jitegemee na kuongozwa na Mkuu huyo wa wilaya na wananchi wakiwemo viongozi wa dini.

Alisema wananchi wa wilaya hiyo walikuwa wakimuona hayati Mkapa akipita wilayani humo akitokea uwanja wa ndege Jijini Tanga kuelekea Lushoto na kwa sasa hawawezi kumuona tena hivyo waendelee kumuenzi ikiwemo kumuombea.

“Ndugu zangu wana Muheza tulikuwa tunamuona Hayati Mkapa akipita hapa kwetu akitokea uwanja wa ndege Tanga na kuelekea wilayani Lushoto na sasa hatutamuona tena hiyo tuendelee kumuombea mwenyezi Mungu”Alisema DC

“Lakini Hayati Mkapa aliwapika aliwapika uji akaweka sukari na bluu bendi na kuwanywesha hivyo wanamuombea kwa mola aweze kumuweka mahali pema peponi amani “Alisema DC Mhandisi Mwanasha.

Alisema kwamba msiba huo ni wa watu wote na Rais Magufuli yupo kwenye wakati mgumu hivyo tuendeleze maombi ambayo yatakuwa ni faraja kubwa sana kwao hasa katika kipindi hiki kigumu.


Hata hivyo alisema kwamba wao kama wilaya wanatoa salamu za pole na kumuomba mola azidi kuwapa faraja katika kipindi hiki kigumu huku akiwapa pole familia ya hayati Mkapa .

Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu alisema kwamba mwenyezi Mungu amemchukua Rais Mstaafu Benjamini Mkapa wakati bado mchango wake ulikuwa ukihitajika kwenye Taifa huku akiwataka watanzania kuendelea kumombea.

Alisema kwamba watanzania bado walikuwa wakimuhitaji hayati Mkapa ambaye alikuwa ni mtu wa uwazi kwa kutaka maendeleo na kuhakikisha anawainua wanyonge na watu wa chini ili waweze kunufaika.

“Kwa kweli kuondoka kwa Rais Mstaafu Benjamini Mkapa ni pengo na litakuwa ni ngumu sana kuzibika kwa sababu alikuwa ni mtu wa uwazi na ukweli ikiwemo kutaka maendeleo”Alisema

Mkuu huyu wa wilaya alisema Mkapa alikuwa ni kiongozi mpiganaji ambaye hakusita kujenga hoja na kuitetea hata wakati alipoondoka madarakani bado alikuwa na msaada.
Share To:

Post A Comment: