Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mh Angellah Kairuki akizungumza na uongozi kampuni ya Tanelec Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji,Mh Angellah Kairuki akipanda mti wa kumbukumbu  katika viwanja vya kiwanda cha Tanelec kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kanani Kihongosi akichota udongo.

 Baadhi ya mafundi wa kiwanda cha Tanelec wakiwa katika utengenezaji wa Transfoma.


Na Lucas Myovela_Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji,Mh Angellah Kairuki ameitaka kampuni ya Tanelec inayozalisha transfoma za umeme  katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhakikisha inaendelea kujitangaza zaidi sambamba na kupata masoko ili kuongeza tija katika ukuaji wa uchumi.

Kairuki aliyasema hayo wakati alipo fanya ziara yake ya kikazi katika  kiwanda hicho kilichopo Jiji Arusha  kwaajili ya kujiinea shughuli mbali za uzalishaji wa transfoma pamoja na kusikiliza changamoto zinawazo wakumba katika uzalishaji wa transfoma hizo za kisasa.

Kairuki ameeleza kuwa kampuni hiyo ambayo ni mbia na serikali ihakikishe  inajitahidi  kutengeneza transfoma nyingi kwaajili ya kuwezesha Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kusambaza umeme hadi kufikia Juni 29 mwaka huu kwani serikali ya awamu ya tano imefanikisha kusambaza umeme kwa  vijiji 9,314  ikilinganishwa na vijiji 2018 vilivyokuwa vimeunganishwa umeme kwa mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 361.5 kupitia mpango kabambe wa usambazaji umeme vijijini. 

"Tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani hadi leo hii wateja zaidi ya milioni 2.7 wamepata umeme sawa na ongezeko la asilimia 361.5 niwaombe muendelee kufanya tafiti za kimasoko  ili kuona uhitaji wa transfoma mbali mbali katika nchi za EAC pamoja na nchi nyingine ili kuuza transfoma hizi zinazo tengenezwa Nchini kwetu Tanzania",ameeleza Kairuki.

Awali Mkurugenzi wa Tanelec, Zahir Saleh alisema changamoto kubwa inayo wa kabili ni ununuzi wa waya aina ya enamael  kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa ingawa hapa nchini Tanzania kunaviwanda vinne vinavyotengeneza waya ila hawatengenezi waya aina hiyo ndio maana wanaagiza nje ya nchi.

Aidha Zahir aliomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuondoa urasimu wa kodi mbalimbali pale wanapoingiza bidhaa kutoka nje y nchi kwaajili ya kutengeneza transfoma nchini ni kuishukuru serikali kushirikiana kwa pamoja katika kuendesha kiwanda hicho kwani hivi sasa tangu kuanzishwa kwa viwanda vingi awamu hii ya tano wamiliki wa viwanda mbalimbali vilivyopo nchini wanaona mafanikio.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi alimshukuru uwepo wa kiwanda hicho ikiwemo kusambaza transfoma zaidi katika miradi mbalimbali Rea iliyopo vijiji mbalimbali nchini na mijini.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: