Na Allawi Kaboyo Bukoba.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera kamishina msaidizi wa polisi Revocatus Malimi leo juni 02,2020 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa shirika la elimu ya Amani Tanzania kwa lengo la kuzungumzia masuala mazima ya Amani mkoani humo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake, Kamanda Malimi ameeleza hali ya Amani na usalama ndani ya mkoa wake ambao amesema kuwa mpaka sasa hali ni shwari na kuongeza kuwa hakuna matukio ya kihalifu hasa ya kutumia silaha na wamejitahidi kupambana na hali hiyo na sasa watanznaia wa Kagera wananishi kwa Amani.
Malimi amelitaka shirika hilo kuzingatia kanuni na taratibu za nchi katika kutekeleza majukumu yake huku akiahidi kutoa ushirikiano wakati wowote atakapohitajika na kuongeza kuwa uwepo wa wadau hao wa Amani ni jambo muhimu sana katika kuelimisha jamii hali inayoweza kuwapelekea wananchi kucha vitendo vy kihalifu.
“Kagera ni mkoa wenye Amani na tunaendelea kuhubiri hilo, niwaombe ndugu zangu nyinyi ni wadau wakubwa kwetu na tunawahitaji sana, jukumu letu sisi kama jeshi la polisi ni kusimamia sharia na kulinda Raia na mali zake, hivyo niwaondoe wasiwasi katika utekelezaji wa majukumu yenu jeshi la polisi Kagera litatoa ushirikiano mkubwa lakini pia niwaombe tuzingatie taratibu na kanuni za nchi yetu.” Amesema Kamanda Malimi.
Kwaupande wake Rais wa shirika la elimu ya Amani Tanzania Ndg.Wilson George amesema kuwa jeshi la polisi ndio wadau namba moja wa shirika hilo na kumueleza kamanda huyo kuwa ujio wa shirika hilo ofisini kwake ni kuta kujitambulisha licha ya kuwa tayari jeshi hilo makao makuu wanawatambua na kuwapa ushirikiano.
Ameongeza kuwa lengo la shirika hilo ni kuhakikisha watanzania wote wanatambua maana halisi ya neon Amani na nini kinaweza kutokea pindi Amani itakapotoweka pamoja na gharama za kuirejesha ambapo pia amesisitiza kuwa kushirikiana na jeshi la polisi ni kutaka jamii kutolichukulia jeshi hilo kama adui kwao.
“Wadau wetu wakubwa ni jeshi la polisi na mwanachama namba moja ni mkuu wa polisi Tanznaia afande Siro, amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa kwetu nikuombe kamanda wetu wewe uwe kiunganishi chetu kwa jamii, tunataka baada ya miaka kadhaa Tanzania kila mtu aaze kulala mlango wazi akiwa hana hofu ya kuvamiwa au kuibiwa endappo watanzania watajua elimu ya Amani na viashairia vya uvunjifu wa Amani.” Amesema Rais George.
Aidha Rais huyo amekutana na kuzungumza na kamanda wa polisi wa wilaya Bukoba mrakibu wa polisi Babu Sanale ambapo amemueleza kuwa shirika lina malengo ya kufanya mambo makubwa katika wilaya hiyo na kikubwa alichokiomba ni ushirikiano kutoka kwake na vijana wake.
Kamanda Sanale amemuhakikishia Rais huyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa kushiriki semina na matamasha yatakayotolewa na shirika hilo kwa nia ya kutoa elimu ya amni kwa wanabukoba na kwa jeshi la polisi kwa kufata misingi ya Amani hapa nchini.
“Sisi tupo tayari kutoa ushirikiano mkubwa kwenu kwanza kwa kutoa ulinzi pale utakapohitajika kama mtafanya mikutano lakini kushiriki kikamilifu utoaji wa elimu ya Amani kwa watanzania, ombi langu kwa wananchi wa Bukoba kutoa ushirikiano mkubwa kwa shirika hilo ili kuhakikisha elimu ya Amani inamfikia kila mmoja na kwa usahihi.” Amesema OCD SANALE.
Shirika la elimu ya Amani Tanzania linaendelea na ziara yake mkoani Kagera yenye lengo la kujitambulisha kwa wadau muhimu wa masuala ya Amani ambapo leo juni 02,2020 ziara hiyo itakuwa wilaya ya Bukoba.



Share To:

Post A Comment: