Rafiki, safari ya kuelekea kwenye mafanikio inaendelea, uamuzi bado unabaki kuwa mikononi mwako. Kila mtu anatamani kufanikiwa, lakini ni wachache sana wanao weza kufikia mafanikio wanayo yataka au kuyatamani.

Je ulishawahi kutamani au kupanga kupiga hatua katika maisha yako, lakini ukashindwa? Je ulishawahi kutaka au kutamani kubadilisha tabia mbaya lakini ukaishia kushindwa? Unatamani kuachana na mzigo wa madeni lakini kila ukijaribu kujinasua unashindwa? Rafiki, nimekuuliza haya maswali si kwa nia mbaya bali ni kutaka kukuleta karibu kwenye tafakari yetu ya leo.

Waingereza wana msemo wao maarufu kuwa “Kama unataka kuendelea kupata kile unachopata basi endelea kufanya kile unachokifanya”. Kuna ukweli katika msemo huu, na hapo ndipo watu wengi huwa wanakwama. Watu wengi wanataka mafanikio, lakini huku wanaendelea kufanya mambo yaleyale wakitegemea wapate mafanikio. Watu wengi wanataka kubadirisha maisha wanayoishi ya umasikini lakini wanaendelea kufanya yaleyale kwa njia zile zile.

Rafiki kuna njia moja tu ya kukuwezesha kupata hayo mafanikio au mabadiriko unayoyataka, nayo ni KUACHA. Ndiyo, ni KUACHA.

Kama wewe siyo tajiri na unataka kuwa tajiri, ACHA kufanya kile unachofanya kila siku, badala yake fanya kwa utofauti na ulivyozoea kufanya. Kama ulikuwa ukitumia hela bila mpangilio au mpango ACHA, na badala yake, kuwa na mpango wako juu ya fedha yako. Kwa kuacha kufanya kile ambacho umezoea kufanya juu ya fedha yako, ni njia rahisi yawewe kujinasua na kutoka kwenye umasikini. Kwani hutapata tena kile ambacho umezoea kupata. Lakini kama umeridhika na kile unachokipata basi endelea kufanya kile uchokifanya.

Njia hii ya kuacha kufanya kile unachokifanya siyo tu itakupa matokea unayoyahitaji bali pia itakufanya uwe watofauti. inatengemea na tatizo ulilionalo, kama haulizishwi na jambo lolote kwenye maisha yako, basi unatakiwa uache kufanya kama ambavyo umezoea kufanya, fanya kwa utofati. Watu wengi huwa hawako tayari kuacha kufanya vile walivyozoea kufanya,ili hali wanataka mafanikio.

Kama unamaarifa kidogo juu ya jambo fulani, na ulikuwa hujifunzi, basi anzakujifunza, soma vitabu juu ya hilo eneo, hudhuria semina achana na mambo yote yanayo kupotezea muda na weka nguvu zako kwenye kujifunza zaidi na zaidi. Kwa kuachana na namna ulivyokuwa umezoea kufanya (kutokusoma, kutokujifunza juu ya hilo eneo), siyo tu utaweza bali pia utakuwa mtu wa tofauti na hapo awali.

Hivyo rafiki, kama unataka kubadiri maisha yako haikikisha huendelei kufanya yale yale uliyozoea kufanya ambayo ndiyo huwa yanakupa matokeo ambayo huyahitaji. Lakini kama unataka kuendelea kupata kile unachopata kila siku basi endelea kufanya vile vile unavyofanya, uamuzi unabaki mikononi mwako.

Ukawe na siku njema rafiki, unapokwenda kufanya maamuzi mazuri juu ya maisha yako leo, kuendelea kupata kilekile unachokipata ama kuachana na yaleyote uliyozoea kuyafanya na badala yake, ufanye kwa utofauti ili kupata matokeo unayoyahitaji. Pia Ili kuendelea kupata makala hizi na huduma zetu kwenye emaili yako jiandikishe hapa chini.
Share To:

Post A Comment: