Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Singida mjini wakimpongeza Rehema James (katikati) baada ya kuchaguliwa na mkutano mkuu wa chama hicho kugombea nafasi ya ubunge mjini hapa jana.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Singida, Emmanuel Jingu akiwahutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho kabla ya kuanza uchaguzi wa wagombea nafasi za ubunge.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (CHADEMA) Josephine Lemoyan, akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
 Wajumbe wakiwa kwenye  mkutano huo.
  Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Singida, Mutta Adrian akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
  Wajumbe wakiwa kwenye  mkutano huo. 
 Wagombea nafasi ya ubunge wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Noela Lemoyan , Rehema James, Shwahibu Mohamed na Aisha Luja.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Jimbo la Singida mjini, Rumbaeli Mjengi akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Mgombea Aisha Luja akiomba kura kwa wajumbe.
 Mgombea Noela Lemoyan akiomba kura kwa wajumbe.
Wajumbe wakitoka kwenye mkutano huo.



Na Waandishi Wetu, Singida

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Singida Mjini mkoani Singida kupitia mkutano mkuu maalumu wa jimbo umemchagua Rehema James kuwa mgombea ubunge na ubunge viti maalumu ili kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu.

Wagombea katika nafasi hizo za uwakilishi wa wanawake yaani ubunge viti maalumu na jimbo katika mkutano huo uliofanyika jana walikuwa ni Shwahibu Mohamed,Rehema James,Aisha Luja pamoja na Noela Lemoyan.

Katika uchaguzi huo nafasi ya ubunge aliyeibuka kidedea ni Rehema James ambaye alipata kura 99 akifuatiwa na Shwahibu Mohamed ambaye alipata kura 51 na Noela Lemoyan akipata kura 13.

Kwa upande wa ubunge viti maalumu Rehema James aliwabwaga tena wagombea wenzake kwa kuibuka na kura 34 sawa na 62.92% akifuatiwa na Aisha Luja kura 16 sawa na 29.62% huku Noela Lemoyan akipata kura 3 sawa na 7.46%.

Baada ya kuchaguliwa mgombea huyo ngazi ya Wilaya,jina lake litapelekwa ngazi ya taifa ili kupitishwa kuwa ndiye mgombea rasmi wa chama hicho na kuipeperusha bendera ya Chadema.


Wajumbe walioshiriki uchaguzi huo ni makatibu kata,wawakilishi mkutano mkuu kata kuja Jimbo, Makatibu wenezi kata,Wenyeviti na Makatibu kata wa baraza la Vijana (Bavicha), Wenyeviti na Makatibu kata Baraza la wazee (Bazecha).

Wengine ni Wenyeviti na Makatibu kata Baraza la wanawake (Bawacha), wawakilishi Baraza la wanawake wanne kutoka kila kata pamoja na wajumbe 15 kutoka kamati tendaji Wilaya.

Awali akifungua Mkutano huo mwenyekiti wa chama hicho Mkoa Emanuel Jingu aliwataka wajumbe hao kuwachagua wagombea hao wenye sifa ambao watakipa ushindi chama hicho na kuvibwaga vyama vingine ikiwemo CCM.


"Tuhakikishe tunamchagua kiongozi mzuri ambaye atakiletea ushindi chama chetu na kikiondoa chama cha Mapinduzi CCM." alisema mwenyekiti huyo.

Share To:

Post A Comment: