Na Mwandishi Wetu 


WAZIRI  wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametengua uteuzi wa Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dk. Sophia Mlote kufuatia kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.

Mabadiliko hayo yamekuja  siku chache baada ya Waziri Mpina kufanya ziara ya kushtukiza saa 10 usiku  katika eneo Ubungo wanakouza maziwa wajasiriamali wadogo na kupokea malalamiko ya wajasirimali hao kuharibiwa maziwa yao kwa kuwekewa rangi na Mafuta ya taa na baadhi ya maofisa wa Bodi ya Maziwa .

Hata hivyo Waziri Mpina aliagiza Maofisa wa Bodi ya Maziwa kusitisha mara moja operesheni ya kuharibu maziwa ya wananchi na kutaka hatua za haraka zichukuliwe kuwaelimisha namna bora ya kufanya biashara hiyo badala ya kuchukua uamuzi wa kuharibu maziwa yao kwa rangi na Mafuta ya taa.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo Serikalini, Elibariki Mafole imesema uamuzi uliofanywa na Waziri Mpina ni kwa mujibu wa   mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Maziwa namba 8 ya mwaka 2004.

Taarifa hiyo  imesema kuwa  uteuzi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa Utafanyika hapo baadae.

Hata hivyo baada ya Waziri Mpina kufika eneo hilo la Ubungo alihoji hatua ya kuharibu maziwa ya wananchi kwa kuweka rangi na Mafuta ya taa  iliyofanywa na Bodi ya Maziwa ulizingatia Kanuni gani jambo ambalo maofisa wa Bodi hiyo walioshindwa kuonesha kifungu kinachowapa mamlaka ya kupima maziwa kwa macho na kuweka mafuta ya taa.

Mmoja wa wafanyabiashara wa Maziwa, Ester Elius alisema zoezi hilo lililofanywa la kuwawekea mafuta ya taa rangi kwenye maziwa limewapatia hasara kubwa na kuomba Serikali kuwasaidia mikopo ili waweze kukidhi matakwa ya kisheria yanayotakiwa na bodi hiyo badala ya 

Hivyo Waziri Mpina  aliagiza Mratibu wa Dawati la Sekta Binafsi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Stephen Michael kukutana na wajasirimali hao ili kutambua mahitaji yao ya kifedha na kuwaunganisha na Taasisi za kifedha kwa ajili ya kupatiwa mikopo ili waweze kufanya biashara zao kwa tija.

Afisa wa Bodi ya Maziwa, Justa Kashumba alisema hatua walizochukua kuharibu maziwa hayo zipo kwa mujibu wa Kanuni huku akishindwa kumuonesha Kanuni iliyotumika Waziri Mpina.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: