Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameagiza kukamilishwa kwa soko la Manispaa ya Morogoro ifikapo June 17 mwaka huu. Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa katika ziara ya kikazi Mkoani Morogoro kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya Ofisi hiyo. Agizo hilo amelitoa kutokana na kuchelewa kukamilika soko hilo ndani ya muda uliopangwa awali. Soko hilo ndio soko kubwa la bidhaa kupitia fedha za miradi ya  kimkakati hapa nchini lilioanza kujengwa mwanzoni mwa mwaka wa jana ambalo litawezesha wafanya biashara kupata mazingira rafiki ya kufanyia biashara.

Pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa soko la Manispaa ya Morogoro Jafo alifanikiwa kutembelea ujenzi wa standi ya daladala ya Mafiga inayojengwa chini ya usimamizi wa TARURA kwaajili matumizi ya Manispaa hiyo ya Morogoro ambapo Waziri huyo alifurahishwa sana na kasi ya ujenzi wa standi hiyo fikia wastani wa asilimia 98 ya ujenzi.

Aidha,  Jafo ameitaka Manispaa hiyo kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo vyake mbali bali vikiwemo masoko na standi za mabasi ili kuongeza pato la Manispaa hiyo.
Share To:

Post A Comment: