Image may contain: 16 people, people standing and outdoorNa John Walter-Babati

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), leo june 13,2020 imewajengea uwezo watumishi wa TRA mkoani hapo kwa kuwapatia semina ya siku moja juu ya maadili na uadilifu katika utumishi wa Umma.

Sultani Ng'aladizi mkuu wa dawati la Elimu kwa Umma kutoka TAKUKURU Mkoani Manyara, aliongoza Semina hiyo iliyofanyika katika Ofisi za TRA zilizopo mtaa wa Miomboni mjini Babati.

Semina hiyo ilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa TRA Makao Makuu na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Holle Makungu.

Semina hiyo imekuja wakati ambao watumishi watano wa Mamlaka ya mapato mkoani Manyara wanakabiliwa na tuhuma za kuomba na kupokea Rushwa kutoka kwa wafanyabiashara.

Hata hivyo Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara Holle Makungu amesema elimu wanayoitoa kwa jamii imeanza kuzaa matunda ambapo kwa sasa kumekuwa na muamko mkubwa katika kuripoti vitendo vya rushwa, hatua inayosaidia wahusika kubainika haraka.

Share To:

Post A Comment: