Na Ferdinand Shayo,Manyara.

Kampuni ya Mati Super Brand imekabidhi vifaa vya kujikinga na Corona ikiwemo,vitakasa mikono ,sabuni maalumu za kunawa pamoja na vyakula kwa makundi ya wazee wasiojiweza pamoja na watoto yatima.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brand David Mulukozi  akikabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti ,alisema kuwa msaada huo utawayasaidia makundi mbalimbali kupambana na Corona ikiwemo taasisi za serikali kama Polisi,Magereza,Wauguzi ambao wanaudumia watu wengi.

Mulokozi alisema kuwa licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona wadau wa maendeleo wanaungana na serikali kuhakikisha kuwa juhudi hizo zinaendelea kuleta mafanikio makubwa.

”Hatujayasahau makundi maalumu ya watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu na wazee ,tumewapatia vitakasa mikono pamoja na vyakula ili viweze kuwasaidia katika kipindi  hiki”Alisema Mulokozi

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akipokea vifaa hivyo alisema kuwa licha ya kuwa mkoa huo uko salama bado wananchi wanapaswa kuendelea  kuchukua tahadhari na kuhakikisha kuwa wanajikinga na kujilinda na ugonjwa huo

Mnyeti aliwapongeza wadau hao kwa kujitoa kusaidia jamii na kuwataka wadau wengine na makumpuni kuiga mfano  kwa kuijali jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wapokeaji wa Msaada huo Samson Munuo alisema kuwa misaada hiyo itatumika vyema kuhakikisha walengwa wanajilinda na kujikinga na ugonjwa wa Corona ili waweze kuchangia katika ujenzi wa taifa na kuendeleza shughuli za kila siku.
Share To:

Post A Comment: