Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amefurahishwa na utendaji kazi wa Viongozi na watendaji wa Mkoa na Jiji la Mbeya  kwa kusimamia kazi bila kufanya maigizo. 

Jafo aliyasema hayo wakati wa Ziara ya kikazi aliyoifanya Mkoani humo leo hii akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika ziara hiyo Waziri Jafo alikagua na kuweka jiwe la msingi ya shule mpya ya Msingi iitwayo Magufuli inayojengwa katika jiji la Mbeya, ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, pamoja na ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya Mbeya.

Mkoa wa Mbeya umepokea shilingi bilion 2.1 kwaajili ya kuanza ujenzi wa Ofisi ya Mkoa, shilingi milion 790 kwaajili ya ukarabati wa shule kongwe ya Mbeya ambapo kazi hizo zote zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Akiongea na wanafunzi wa kidato cha sita wa sekondari ya Mbeya waliorejea shuleni hapo leo hii kwa maelekezo ya Serikali, Waziri Jafo amewataka wanafunzi hao kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo yote yaliyo tolewa na serikali juu ya kujilinda na janga la korona huku wakijiandaa na maandalizi ya mitihani yao itakayoanza ndani ya mwezi huu wa Juni.
Share To:

Post A Comment: