NA HERI SHAABAN
HALMASHAURI ya Manispaa Ilala yapiga marufuku  Mamalishe na Baba Lishe kutumia vyombo vya plastiki.

Hayo yalisemwa na Afisa Afya wa Manispaa hiyo Reginald Mlay wakati wa semina ya Mamalishe wa manispaa hiyo kutoka kata TABATA, Mchikichini, Kivukoni, Kiwalani, iliyofanyika wilayani Ilala Leo.

Reginald alisema vyombo vya plastiki katika matumizi ya chakula sio salama zinasababisha kushika uchafu haraka pia si salama kwa matumizi ya chakula cha moto.

"Mama Lishe na Baba Lishe marufuku kutumia vyombo vya plastiki na mifuko ya Rambo si salama kwa kuifadhia chakula cha moto kwa sababu kuna viambata vinavyoleta athari katika mwili kupelekea kupata kansa kwa watumiaji wa vyombo hivyo" alisema Reginald.


Reginald alisema mafunzo haya ya Mama Lishe wa halmashauri ya Ilala ni endelevu yameandaliwa na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa   ya Ilala kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi ambapo kila mwaka tunawapatia elimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo sekta yao itambulike.

Aidha alisema kabla kuwapatia elimu hiyo walifanya ukaguzi manispaa yote kwa ajili ya  kuwapima afya lengo kujua afya zao waweze kutoa huduma safi na Salama  hata chakula kinachoandaliwa kiwe safi kisichafuliwe wakati wa maandalizi.

Kwa upande wake Afisa Lishe Manispaa ya Ilala Frola Mgimba alisema dhumuni la mafunzo hayo kuwajengea uwezo wa kazi yao itambulike.

Pia Frola alisema sekta ya Mama Lishe na baba Lishe ni sekta muhimu mafunzo hayo yanawasaidia waweze kuandaa mlo kamili kwa afya za walaji kwani asilimia kubwa mlo wa mchana wanategemewa Baba Lishe na Mama Lishe hivyo waweke vyakula vya ziada.

Naye Irene Munishi Mama Lishe TABATA alisema mafunzo hayo yamewajengea uwezo  wawapo kazini  katika kuwahudumia wateja.

Irene alisema sekta ya Mama Lishe na Baba Lishe mazingira yao katika eneo wanalopangiwa si rafiki, wameiomba halmashauri ya ILALA kuwajengea utaratibu mzuri wa kazi yao wawapo eneo la kutolea huduma.

MWISHO
Mafunzo ILALA
Juni 28/2020
Share To:

Post A Comment: