Monday, 1 June 2020

Ikizu Pharmacy watoa msaada wa Vifaa Kinga kwa Waandishi wa Habari.


Na John Walter-Babati
Mdau wa Maendeleo mkoa wa Manyara (IKIZU PHARMACY) ambayo inashughulika na kutoa huduma za afya kwa kuuza dawa za Binadamu, ametoa msaada wa vifaa vya kinga vya corona kwa waandishi wa Habari mkoa wa Manyara.
Akitoa msaada huo mwakilishi kutoka Ikizu Pharmacy Wilson Mbogo,  amesema wameamua kuwapatia waandishi wa habari msaada huo ili waweze kufanya kazi zao kwa uhuru na salama.
Mbogo amesema kuwa msaada walioutoa kwa ajili ya kuwasaidia waandishi wa habari katika kipindi hiki cha mlipuko wa homa ya mapafu (COVID19) una thamani ya shilingi laki sita na sitini elfu.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Manyara Yusufu Daiy amesema misaada walioipokea ni Vitakasa Mikono,Sabuni za mikono,Gloves pamoja na barakoa.
Katibu wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Manyara (MANYARA PRESS CLUB) Thedy Challe amemshukuru mdau huyo huku akiahidi kugawa msaada huo kwa waandishi kama ilivyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment