Na Ahmed Mahmoud Arusha
MKUU wa Wilaya ya Arusha Gqbriel Daqarro jana amekabidhi hundi ya zaidi ya Sh.milioni 626 kwa vikundi 100 vya watu wenye
ulemavu,wanawake na vijana ili waendelee kufanya biashara zao bila kukwama.

Akikabidhi hundi hiyo jana jijini Arusha,alisema fedha  hizo zinatokana na mapato ya fedha za ndani za jiji hilo.

"Mikopo hii zamani watu walikuwa hawazipati lakini kutokana na Rais John magufuli kusema asilimia hii ipelekwe kwa watu wake ndio maana halmashuri zinatenga na kuwapa wahusika hao,"alisema.

Aidha alisema fedha hizo ziliombwa na vikundi 109, lakini  tisa kati ya hivyo hazijapata sababu wamekosa sifa, hivyo aliomba wahusika wa mikopo waelekeze vikundi hivyo ili waendelee kufanya vizuri na awamu ijayo vipewe kipaumbele.

Aliwataka wanakopeshwa fedha hizo ziwasaidie kukua kiuchumi kwa kupiga hatua katika biashara zao na kuepuka kuzipeleka kwenye matumizi yasiokusudiwa.

Pia aliwataka Maofisa Maendeleo Kata kusimamia vizuri vikundi hivyo pamoja na kuelekeza aina za biashara za kufanya amabzao zitawazalishia fedha badala ya kuvitelekeza.

"Naomba pia awamu ijayo tuone vikundi vingi zaidi vya watu wenye ulemavu na tusiwabague ili nao wanufaike na mikopo hiyo na wengi
wakisaidiwa wanaachana na omba omba na wanauwezo wa kufanya biashara,"alisema.

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,  Mwanamsiu Dossi, alisema fedha hizo zimetokana na urejeshaji wa zaidi ya Sh.milioni 122.2 wa vikundi vilivyokopeshwa  na zaidi ya Sh.milioni 504.6 zimetokana na fedha za mapato ya ndani.

Alisema mikopo hiyo iliyotolewa  zaidi ya Sh.milioni 626.8 kati ya
hizo Sh.milioni 377 zimetolewa kwa vikundi 65 vya wanawake,Sh.milioni 234.866 vikundi 32 vya vijana na Sh.milioni 15 vikundi vitatu  vya watu wenye ulemavu.

Alisema halmashauri itaendelea kutoa mikopo hiyo kadiri itakavyokuwa ikitolewa maombi kutoka kwenye vikundi kulingana na fedha zitavyopatikana kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani na marejesho ya mikopo ya nyuma.

Mkurugenzi wa Halmashuri ya Jiji la Arusha Dk.Maulid Madeni amemwomba Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro  kuongeza kiwango cha fedha za kukopesha kwa walengwa hao ili ziwasaidie kufanya biashara.

"Sio lazima tuwape fedha tunawezabkuboresha kwa kununua mashine za kufyatulia tofauti vijana na akna mama wapewe mashine za kushona nguo wakaongeza kipato kwa bidhaa watakazozalisha,"alisema.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Denisi  Zakaria amevitaka vikundi vya wanawake,vijana na walemavu wanaokopeshwa fedha na serikali wazirejeshe kwa wakati ili wenzao wapate.

Alipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuhakikisha asilimia kumi ya mapato yake ya ndani wanawapa makundi hayo tofauti na
halmashutinzingine nchini wanazitenga na kuzifanyia kazi zingine nje ya ilivyokudiwa.

"Lakini sababu sisi CCM tuwakuna kwa kuwapa fedha za mikopo nanyi mtukune wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu,"alisema.


Share To:

Post A Comment: