Burundi imemuapisha rais mpya wa taifa hilo , Evariste Ndayishimiye, katika hafla iliofanyika mbele ya raia wa taifa hilo na baadhi ya viongozi kutoka mataifa tofauti.

Katika kiapo chake rais huyo ameapa kulinda katiba ya Burundi, kuheshimu umoja wa raia wa taifa hilo, kutoa haki kwa wote mbali na kutetea mipaka ya taifa hilo.

Sherehe hiyo iliofanyika katika uwanja wa kandanda wa Ingoma katika mkoa wa Gitega imefanyika wakati ambapo taifa hilo limeathirika na mlipuko wa vurusi vya corona.

Rais Evariste baada ya kumaliza kula kiapo alkagua gwaride la kijeshi na baadaye kutoa hotuba .
Share To:

Post A Comment: