Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega na kaim Mganga wa mkoa wa Arusha Dkt.Omary Shariff wakipokea vitakasa mikono lita 500 vilivyotolewa na Kampuni ya Bia ya TBL leo kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea Mara baada ya kupokea vitakasa mikono kutoka kwa Meneja Uzalishaji wa kiwanda Cha bia Joseph Mwaikasu Leo jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

Meneja Uzalishaji wa kiwanda Cha bia TBL Joseph Mwaikasu akiongea kwenye hafla ya makabidhiano ya vitakasa mikono vilivyotolewa na Kampuni ya Bia ya TBL leo kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha

Sehemu ya wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya TBL wakifuatilia hafla hiyo wakati wakikabidhi kwa Serikali vitakasa mikono lita 500 Leo jijini Arusha .

Sehemu ya shehena ya vitakasa mikono iliyotolewa na kiwanda Cha bia TBL kwa Serikali mkoani hapa ikiwa ni kuendeleza mapambano dhidi ya Ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha



Na Ahmed Mahmoud,,Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema ataishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuondoa utaratibu wa sasa wa kuwaweka kwenye karantini ya siku 14 wageni wote wanaoingia mkoani hapa kwa shughuli za utalii ili kuepusha kuwakatisha tamaa.

Gambo amelazimika kutoa kauli hiyo mapema leo wakati akipokea msaada wa Lita 500 za vitakasa mikono kutoka kampuni ya bia nchini, TBL na kueleza kwamba njia sahihi ya kuendelea kuchapa kazi ni pamoja na kuruhusu watalii walioonyesha nia kuingia nchini kama njia moja wapo ya kuvutia utalii .

Alisema wapo wageni wengi walioonyesha nia ya kutembelea vivutio mbalimbali mkoani hapa ila wanakumbwa na kikwazo cha Karantini jambo linalowakatisha tamaa na hivyo ameonelea ipo haja ya kuishauri serikali kubadilisha kipengere hicho ili kuangalia namna nzuri zaidi itakayowapendeza watalii bila kueneza maambukizo ya Korona.

Amesema sekta ya utalii ni muhimu sana kwa ustawi wa mkoa wa Arusha hivyo ameonelea ipo haja kwa watalii walioonyesha nia yakuingia nchini kuanzia mwezi juni mwaka huu kupewa utaratibu mpya wa maambukizi ya ugonjwa wa Korona badala ya kuwekwa kwenye Karantini ambayo huwapotezea muda na kuwaongezea gharama zaidi.

"Tunafikiria mkoa wa Arusha kuishauri serikali ili kile kipengere cha Karantini iweze kukiondoa ili kuepuka kuwakatisha tamaa watalii walioonyesha nia ya kuja mkoani hapa kuanzia mwezi juni mwaka huu"Amesema Gambo

Katika hatua nyingine Gambo alisema kuwa mkoa wa Arusha utaendelea kutoa elimu kwa wananchi sanjari na kuwaondoa hofu ikiwemo kuondoa misongamano isiyo ya lazima kwa kuweka utaratibu wa mazishi kwa watu wasiozidi 10 na kuwa sio kila anayefariki basi amefariki wa Ugonjwa wa Covid 19.

Awali Meneja Uzalishaji wa kiwanda Cha bia cha TBL ,Joseph Mwaikasu alisema kampuni imeona uhitaji wa jamii na kuunga Juhudi za Serikali za kukabiliana na Ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 kwani hata wafanyakazi wao idadi kubwa ni wakazi wa mkoa wa Arusha.

Alisema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuhakikisha waendelea kusaidia katikamapambano dhidi ya janga hili hatari.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega alizipongeza baadhi ya Taasisi na mashirika mbalimbali ambayo yamekuwa yakitoa vifaa kwa ajili ya kupambana na Ugonjwa huo na kutaka wengine kuendelea kujitokeza kusaidia.
Share To:

Post A Comment: