Mbunge wa jimbo la msalala wilayani KAHAMA  mkoani Shinyanga Ezekiel Magolyo Maige amesikitishwa na kuguswa kutokana kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita Hamim Buzohera Gwiyama.
Akizungumza na mtandao huu Mhe,Maige amesema Marehemu alimfahamu mengi tangu wakiwa Chuo cha IFM.

"Nimeumia Sana na Msiba Huu. Hamim Gwiyama, Rais wangu wa Serikali ya Wanafunzi IFM 1996, Mhasibu (CPA) Mwenzangu, Partner wetu kwenye MGK (Accountants and Auditors) Associates na DC wetu wa Nyang'hwale! Umenisaidia mengi, ulinihamasisha kuingia kwenye siasa!

Uliahidi kunifuata kwenye siasa na kweli ukagombea Ubunge Kasulu Mjini Mwaka 2015.

Ulipoteuliwa kuwa DC Mwaka 2016, ulikuta mradi wa Maji toka Mhangu kuja Bulyanhulu na Bugarama ( Ilogi) ukiwa unasuasua na Acacia wakiwa wametishia kuufuta. Ulinipigia na kuniambia kwa sauti yako nyepesi na ya upole,  "Maige,  I will help you! I won't let this opportunity go". Ulisimama imara  tulikwenda wote Hadi Wizara ya Maji. Tshs 10bn zikapatikana kuongezwa kwenye Tshs 5bn za Acacia mradi ukaanza 2017.

Umekuwa ukiuita mradi huo "our baby" kila tukikutana.

Umekuwa Kaka, rafiki na mentor wangu siku zoteI! Sisi na vijana wako, akina Peter Serukamba, Dr Mpoki Mwafenga, Dr Bernard Kibesse, Dr Fred Msemwa nk tunalia. Ooh No! Too soon!

Kazi ya Mungu Haina Makosa. Pumzika Kaka, comrade na Raafiki!"amesema Maige.
DC Gwiyama amefariki Dunia Leo Mei 7,2020 katika hospitali ya rufaa Bugando alikopelekwa kupata matibabu baada ya kuugua ghafla
Share To:

msumbanews

Post A Comment: