Wednesday, 13 May 2020

Dc Muro azindua kiwanda cha kutengeneza Barakoa
  Pichani mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akikagua baadhi ya barakoa zilizotengenezwa na kiwanda hicho
Na Woinde Shizza, Arumeru.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro  leo amezindua kiwanda kidogo kitakachokuwa kikizalisha Barakoa kwa ajili ya watumishi wa wilaya hiyo katika sekta ya afya. 

Akizindua kiwanda hicho  kidogo cha uzalishaji wa barakoa katika wilaya hiyo kuwa hicho litasaidia kutengeneza barakoa kwaajili ya wafanyakazi wote was halmashauri hiyo.

Alisema kiwanda hicho kitakuwa ni mali ya Serikali na kipo ndani ya hospitali ya Halmashauri ya Meru Tengeru.

" Tunatengeneza barako kwa ajili ya watumishi wetu wote wa sekta ya afya kwa vituo vyetu vya afya na zahanati barakoa hizi zitasaidia kuwakinga ili wasipate ugonjwa huu wa Corona 19," alisema Jerry Muro.
No comments:

Post a Comment