Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT), Dr Elisha Osati

WAZAZi na walezi wameshauriwa kuwalinda watoto wao ili wasiweze kupata maambukizi ya ugonjwa wa covid -19 ambao unaweza kuhatarisha maisha yao.

Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT), Dr Elisha Osati amesema kuwa, mzazi au mlezi ana jukumu la kumlinda mtoto wake ili asiweze kupata maambukizo hayo hasa katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na ugonjwa huo.

"Watoto walio chini ya miaka 8, bado wadogo, wanahitaji msaada wa ulinzi na usalama kutoka kwa wazazi au walezi wao, hivyo basi katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa covid-19, wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha kiwa,watoto wao hawapati maambukizi haya na wanaendelea kuwa salama," amesema Osati.

Akitolea mfano wa mtoto mwenye umri wa chini ya mwaka mmoja ambaye hawezi kufanya chochote bila msaada wa mzazi au mlezi wake,jukumu kubwa la kumlinda ili asiweze kupata maambukizi hayo linabaki kwa mzazi au mlezi.

Ameongeza kuwa, kwa sababu bado anahitaji malezi na makuzi yaliyo salama kutokana na umri wao kuwa mdogo na kwamba hawawezi kujitetea kwa jambo lolote ambalo litaweza kuhatarisha maisha yake.

Amesema kuwa, kutokana na hali hiyo, wazazi au walezi wanapaswa kusikiliza taarifa zinazotolewa na serikali  kuhusiana na ugonjwa huo na kuchukua tahadhari kwao na kwa watoto wao ili wasiweze kupata maambukizi au kuwaambukiza.


"Serikali inatoa taarifa za Mara kwa mara kuhusiana na ugonjwa wa Covid -19, hivyo basi ni muhimu kwa wazazi au walezi kuzifuatilia na kuchukua tahadhari ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza," amesema.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: