Marekani imekua nchi ya kwanza duniani kurekodi zaidi ya vifo 2000 vya virusi vya corona kwa siku moja.

Takwimu kutoka Chuo Kikuu Johns Hopkins zinaonyesha kuwa watu 2,108 wamekufa katika kipindi cha saa 24, huku kukiwa sasa na zaidi ya watu nusu milioni walioambukia virusi hivyo nchini Marekani.

Marekani hivi karibuni inaweza kuipita Italia kwa idadi zaidi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo kote duniani.

Marekani sasa ina takribani vifo 18,693 na idadi ya visa vilivyothibitishwa ni 500,399, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, ambacho ndicho kinachofuatilia takwimu za ugonjwa huo kote duniani.

Italia imeripoti vifo 18,849 huku vifo zaidi ya 102,000 vikiripotiwa kote duniani kutokana na virusi vya corona. 


-BBC
Share To:

msumbanews

Post A Comment: