Katika kuendelez can a jitihada za kuunga mkono serikali katika ulinzi na usalama hapa nchini Mgodi wa Barrick North Mara Mkoani Mara umetoa kontena moja (tupu) kwa Idara ya Uhamiaji  wilayani Butiama Mkoani Mara litakalotumika kama Ofisi ndogo katika Kizuizi cha Kirumi ikiwa na lengo la kurahisisha utendaji kazi katika kizuizi hicho.

Akiongea wakati akipokea kontena hilo Afisa uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna wa Uhamiaji DCI Albert Rwelamila aliwapongeza wakurugenzi wa Barrick North Mara kwa kutoa kontena hilo kwani litasaidia  katika utendaji kazi wa kawaida na kufanya doria za ulinzi imara katika Mipaka ya nchi ili kuendelea kudumisha hali ya amani na usalama wa wananchi na mali zao .

Awali Kizuizi hicho hakikuwa na ofisi au sehemu ya Kutosha  kujikinga na jua au mvua kwa askari wakati wa utekelezaji wa majukmu yao, hivyo kontena hilo limefika wakati muafaka hasa katika kipindi hiki cha kupambana na wahamiaji haramu wanaojaribu kujipenyeza kuingia nchini bila kufuata utaratibu kutokana na ugonjwa wa COVID -19 Unaosababishwa na virusi vya Corona.

Aidha DCI Rwelamila akiwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya ACP William Mkondya waliweza kuongea na askari waliopo katika kizuizi hicho cha Kirumi kwenye barabara ya Sirari-Musoma- Mwanza, walipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi katika vituo mbalimbali vya mipaka na vizuizi Mkoani Mara.

Katika ziara hiyo  walitoa  wito na maelekezo kwa Maafisa na askari wa vituo hivyo juu ya  kushirikiana kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama katika udhibiti wa uingiaji wa wageni nchini kinyume na sheria hasa wakati huu wa juhudi za kupambana na kudhibiti kuenea kwa maambuki ya virusi vya Corona.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: