Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa zungu na Meya wa Ilala wakipanda miti katika uzinduzi wa usafi Tabata Mtambani 
Wananchi wa Tabata Mtambani wakishiriki usafi wa mazingira 
Waziri Zungu na viongozi mbali mbali akijumuika na wananchi wa mtaa wa Mtambani Tabata kufanya usafi 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Zungu amewataka Wananchi wa Tabata kutunza Mazingira yao kwa kupanda miti ili nchi yetu isiwe jangwa.


Waziri wa Mazingira Mussa Zungu aliyasema hayo leo jana wakati akizungumza na wakazi wa Tabata Mtambani wakati  wa uzinduzi wa kampeni ya usafi iliyokwenda sambamba na zoezi la upandaji miti katika mtaa huo wa Mtambani Wilayani Ilala .

"Nawaomba wananchi wa Tabata tutunze mazingira yetu kwa kushiriki usafi pamoja na kupanda miti katika maeneo yote ya Tabata unapokata mti panda mti " alisema Zungu .


Zungu aliwataka Viongozi wa Serikali ya Mtaa na watendaji wa kata hiyo kuwachukulia hatua wachafuzi wa mazingira wanasababisha uharibifu wa vyanzo vya maji.

Alimpongeza balozi wa mazingira mwanahabari Heri Shaaban kwa kufanikisha jambo hilo kuwa  sio dogo ni  jambo kubwa kila mwananchi anatakiwa kuunga mkono .

Katika hatua nyingine waziri wa mazingira alikagua bonde la mto Msimbazi kuangalia athari za bonde hilo ambapo alisema mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus amelizungumzia Bungeni suala la bonde hilo na serikali imeshatenga fedha ujenzi wake unatarajia kuanza hivi karibuni.

Kwa upande wake Meya wa Halmashauri ya Ilala ambaye alikuwa mgeni rasmi Omary Kumbilamoto  aliwapa pole wananchi wa Tabata kwa kupata msiba mkubwa  kata iliyokosa Diwani kupelekea maendeleo kurudi nyuma.

Meya Kumbilamoto aliwataka wakazi wa Tabata wasirudie makosa katika uchaguzi mkuu wachague Diwani ambaye mwenye chachu ya maendeleo ataweza kuunga mkono juhudi za makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utunzaji Mazingira.

Aliwataka wakazi wa Tabata  wasifanye makosa  katika uchaguzi mkuu wachague viongozi wenye chachu ya maendeleo    watakaowezesha kata hiyo kuwa ya kisasa.

Akizingumzia uzinduzi wa mazingira alisema ni utekekezaji  wa agizo la serikali kila mtu jukumu lake kutunza mazingira yanayomzunguka kwa ajili ya usafi

Mratibu wa kampeni hiyo Balozi wa u
safi na Mazingira Heri Shaaban alisema jukumu la utunzaji mazingira ni jukumu letu sote  kila mtu lazima ashiriki usafi.

Balozi Heri Shaaban alisema anaungana na Serikali katika kampeni hiyo endelevu ya utunzaji mazingira  ni muhimu.

"Hewa safi inategemea mazingira safi na salama ikiwemo utunzaji wa miti tukumbuke kupanda miti ya matunda na miti ya kivuli "alisema Heri.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: