Tuesday, 10 March 2020

Waziri Biteko aitaka kampuni ya Noble Helium kuharakisha mradi

Waziri wa Madini, Doto Biteko wa kwanza kulia na wajumbe walioshiriki kikao hicho wakimsikiliza Justyn Wood (wa pili kushoto) akielezea juu ya hatua wliyofikia katika utafiti wa madini ya helium
wajumbe walioshiriki kikao baina ya wizara wakiongozwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa Kwanza kulia) na kampuni ya uchimbaji wa madini ya helium ya Noble Helium kilichofanyika katika ofisi za wizara Mtumba, Jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (kulia) na wajumbe wengine wakifuatilia mada wakati wa kikao hicho. 

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (kulia) akibadilishana mawazo na Wager Jennines pamoja na Justyn Wood kutoka kampuni ya Noble Helium marabaada ya kikao baina ya wizara na kampuni ya Noble Helium kuhitimishwa.
Wajumbe wakipeana mikono mara baada ya kikao baina ya wizara na kampuni ya Noble Helium kwisha.
Waziri wa madini, Doto Biteko (mbele), Naibu waziri, Stanslaus Nyongo ( kushoto) naKatibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (kulia) wakijadili jambo mara baada ya kikao baina ya wizara na kampuni ya Noble Helium kuhitimishwa.
Wager Jennines kutoka kampuni ya Noble Helium akielezea jambo kwa waziri wa Madini Doto Biteko wakati wa kikao baina ya kampuni hiyo na wizara.
Justyn Wood (katikati) akieleza mada wakati wa kikao baina ya kampuni anayoisimamia na wizara.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (kulia) akibadilishana mawazo na wager Jennines baada ya kikao baina ya wizara na kampuni ya Noble Helium kuhitimishwa.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiagana na wajumbe walioshiriki kikao baina ya wizara na kampuni ya Noble Helium mara baada ya kuhitimisha kikao hicho.Na Nuru Mwasampeta, Dodoma

Waziri wa Madini, Doto Biteko leo Machi 10, 2020 amekutana na Wawekezaji wa Kampuni ya Uchimbaji  Madini ya Helium  ya  Noble Helium na kuitaka  kuharakisha Utekelezaji wa mradi huo.

Biteko aliongeza kuwa hakuna serikali duniani isiyohitaji wawekezaji na hivyo basi kutokana na umuhimu na uhitaji wa wawekezaji nchini ni vema wawekezaji kwenda na kasi ya serikali husika ili kupelekea malengo yaliyowekwa na nchi kufikiwa ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Wawekezaji hao walipata leseni ya utafiti wa madini hayo katikati ya mwaka jana (2019) na hivyo kuamua kufika katika Ofisi ya Waziri Biteko ili kueleza hatua waliyofikia katika utafiti wa madini hayo.

Akizungumzia uhakika wa uwepo wa madini hayo nchini, Justyn Wood mmoja wa wajumbe kutoka kampuni ya Noble Helium, amesema  kwa hatua za awali na kwa namna miamba ilivyokaa na jiolojia ya mahala wanapofanyia kazi wana uhakika mkubwa wa uwepo wa kiasi kikubwa cha madini hayo.

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni pamoja   na Viongozi Waandamizi wa wizara pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Dkt. Daniel Budeba.

No comments:

Post a comment