Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga limeipongeza Serikali ya mkoa huo, kupunguza tatizo la mauaji ya wazee pamoja na watu wenye ualbino, ambao walikuwa akiuawa kwa sababu ya imani potofu za kishirikina.
Wazee wametoa pongezi hizo leo Machi 11,2020 kwenye kikao cha Baraza la Wazee Mkoa wa Shinyanga, kilichofanyika kwenye hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinyanga, kilichokuwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi likiwamo suala la matibabu. Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga ,Katibu wa baraza hilo Anderson Lyimo, alisema wanaipongeza Serikali ya mkoa huo kwa kupunguza tatizo la mauaji ya wazee na watu wenye ualbino, ambalo lilikuwa likiwanyima haki zao za kuishi kwa sababu ya watu kuendekeza imani potofu za kishirikina. “Baraza la wazee mkoa wa Shinyanga tunampongeza sana mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, pamoja na watendaji wake, kwa kudumisha amani, utulivu na usalama, pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la mauaji ya wazee na watu wenye ualbino, tofauti na miaka ya nyuma,”alisema Lyimo. “Tunaendelea kuomba juhudi hizi za kutokomeza unyanyasaji, ukatili, na mauaji ya wazee na watu wenye ualbino, ziendelee ili sisi wazee tupate kuishi kwa amani kwenye nchi yetu, pamoja na Serikali kuwachukulia hatua kali watu ambao wanasababisha mauaji ya watu ambao hawana hatia,”aliongeza. Katika hatua nyingine aliiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itunge sheria ya wazee ili watekelezewe masuala yao kwa mujibu wa Sheria , likiwamo suala la upatikanaji wa dawa za wazee, madirisha, madaktari, pamoja na vitambulisho vya matibabu bure, ili waondokane na changamoto za ukosefu wa matibabu. Naye Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, alisema mkoa Shinyanga una jumla ya wazee 66,717, wanaume 29,917, wanawake 36,800, ambapo wazee walio na vitambulisho vya matibabu bure wapo 20,068 na waliokatiwa Bima ya CHF 4,231. Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Nuru Mpuya, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kikao hicho, alisema Serikali itaendelea kutatua changamoto ambazo zinawakabili wa wazee likiwamo suala la matibabu ambalo ndilo changamoto kubwa kwao. TAZAMA PICHA HAPA CHINI Katibu wa baraza la wazee mkoa wa Shinyanga Anderson Lyimo, akisoma taarifa ya utekelezaji wa baraza la wazee mkoa na kuipongeza Serikali kwa kupunguza tatizo la mauaji ya wazee na watu wenye ualbino. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga Faustine Sengerema akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga. Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, akizungumza kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Nuru Mpuya, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga, na kuahidi Serikali itaendelea kukatua changamoto za wazee zinazowakabili. Afisa afya kutoka Ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mussa Makungu, akitoa elimu ya afya kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga ikiwamo namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona. Mwenyekiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Kanda ya Ziwa Ruthi Kanoni, ambaye pia ni muuguzi katika hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinayanga, akitoa elimu kwa wazee hao namma ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kikiwamo Kisukari. Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Katibu wa baraza la wazee manispaa ya Shinyanga Iddi Mpyalimi akichangia mada kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Mratibu wa Shirika la Tawlae linalotetea haki za wazee mkoa wa Shinyanga Eliasenya Nnko, akichangia mada kwenye kikao cha baraza hilo la wazee mkoa wa Shinyanga. Frola Bundala akisoma taarifa ya baraza la Wazee Kahama Mji, kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya ya Kishapu Suzana Masebu akisoma taarifa ya wazee ya wilaya hiyo kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Mwenyekiti wa baraza la wazee halmashauri ya Ushetu Samson Kifutumo, akisoma taarifa ya wazee ya halmashauri hiyo, kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga. Wataalamu wa afya kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza la wazee mkoa wa Shinyanga, wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Kanda ya Ziwa Ruthi Kanoni, ambaye pia ni muuguzi katika hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinayanga, akiwa na Afisa afya kutoka Ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mussa Makungu. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Share To:

Post A Comment: