Na. WAMJW-Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kukabiliana na ugonjwa wga  Corona ili Kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na mheshimiwa WAZIRI Mkuu baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa kinga, fedha na dawa kutoka taasisi, kampuni na umoja wa mama ntilie nchini.

Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema Kuwa Watanzania wanapaswa kuzingatia kuchukua tahadhari kama vile kunawa mikono Mara kwa Mara kwa maji yanayotiririka na kuepuka misongamano ili kudhibiti janga hili kubwa lililozikumba pia mataifa makubwa.

“Wakati tunaendelea kukabiliana na janga hili la Corona pia tunapaswa kujua kwamba ugonjwa huu utaleta athari za kiuchumi,” amesema WAZIRI Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

WAZIRI Mkuu amewashukuru Watanzania waliojitokeza kuchangia fedha, dawa na vifaa kinga kwa Kuwa msaada huo itasaidia watu WOTE waliokumbwa na COVID- 19 pamoja na kusaidia Watanzania kujikinga  ili Kuzuia kusambaa kwa homa kali ya mapafu.

“Hivi vitu vyote tulivyopokea Leo ni gharama kubwa, tumeona Watanzania wenye moyo wamekuja hapa kuungana na Serikali kukabiliana na ugonjwa huu, hivyo hatuwezi kuacha hivi bila kutoa shukrani kwa wenzetu waliotoa msaada huu,” amesema Mhe. Waziri Mkuu.

Amesema Watanzania wanaopenda kuchangia jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu, wachangie fedha Benki Kuu kupitia akaunti ya National Relief Fund Electronic, namba 9921159801 na kwamba wanaweza kuchangia kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Baadhi ya Kampuni zilizochangia Serikali katika kukabiliana na Corona ni Benki ya NMB milioni 100, CRDB  Milioni 150, Benki ya UBA  milioni 230,  umoja wa mama ntilie  Milioni 2, Ashton Media  Milioni 104 na Kampuni mbalimbali zimechangia  fedha na vifaa kinga kwa lengo la kukabiliana ugonjwa wa Corona.

Wakati huohuo Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa kwa kipindi cha masaa 24 tangu jana Alhamisi Machi 27,2020 jumla ya sampuli 26 zimewasilishwa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na zote zimethibitishwa hazina maambukizi'Negative', hivyo  mpaka sasa hapa nchini watu waliothibitika 'positive' kuwa na ugonjwa huo bado ni kumi na tatu(13).

MWISHO
Share To:

msumbanews

Post A Comment: