a Mgamb
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Kiwanda cha Tanga Cement cha Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku sita ambapo alitembelea kiwandani hapo kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa kiwanda hicho Reinhardt Swart kulia ni Waziri wa Madini Dotto Biteko
 Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza wakati wa ziara hiyo
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa kiwanda hicho Reinhardt Swart akizungumza wakati wa ziara hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa ziara hiyo.


SERIKALI imesema kuwa itaendelea kuhakikisha inaweka mazingira  mazuri ya uwekezaji pamoja na kuondoa changamoto zote zinazokwamisha kwa namna moja au nyingine sekta ya uwekezaji nchini.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo leo Jumanne wakati alipotembelea kiwanda cha saruji cha Simba Cement cha  jijini Tanga ambapo alifanya mazungumzo na uongozi pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Amesema kuwa,uzalishaji wa saruji nchini ni mkubwa kiasi kwamba hawawezi kuagiza saruji nje ya nchi kwa kulinda viwanda vya ndani.


“Malengo ya serikali ni kufanya kazi pamoja na wawekezaji kutokana uwekezaji huu una tija kwa serikali kutokana na kodi zinazolipwa na wawekezaji zinasaidia katika kutekeleza kwenye miradi ya maendeleo tunayoiona na kwa upande wa uzalishaji wa saruji tunajitosheleza,ndio maana hatuagizi saruji nje,”alisema.


Aliongeza kwa upande wa changamoto zinazokikabili kiwanda cha Simba Cement amesema atakutana na uongozi wa kiwanda hicho ofisini kwake jijini Dodoma pamoja na mawaziri wenye dhamana za Madini,Uwekezaji,Viwanda pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini(TRC) uongozi wa kiwanda hicho  watoe mapendekezo yao ili waone ni kwa namna gani waweze kuzitatua changamoto hizo.


“Machi 10 ninataka uongozi wa kiwanda cha saruji cha Simba Cement tukutane Dodoma pamoja na Waziri wa madini,Nishati,Viwanda na uwekezaji mlete mapendekezo yenu tuone ni namna gani tunaweza kutatua changamoto zenu kutokana hiki ni moja ya kiwanda kinacholipa vizuri kodi pamoja na kuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi,”alisema.


Alisema kuwa kuhusu changamoto ya usafiri iliyoikumba kiwanda hicho,serikali imeagiza mabehewa 100 na kati ya hayo mabehewa 40 watayaleta katika kiwanda hicho ambacho mahitaji ya mabehewa kwa siku katika kiwanda hicho ni 80 ili kupunguza changamoto ya usafirishaji wa saruji hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.


“serikali imeagiza mabehewa 100 kati ya hayo tutayaleta Simba Cement ili kuondoa changamoto ya usafirishaji,hapa mahitaji ya mabehewa kwa siku ni mabehewa 80,”alisema.


Aidha,kuhusu nishati ya umeme amefafanua kuwa  serikali inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji umeme nchini na muda si mrefu changamoto hiyo itatatuliwa.


Kwa upande wake,waziri wa madini Dotto Biteko,alisema kuwa kiwanda hicho ni moja ya viwanda ambavyo vimekidhi masharti na vigezo vyote vya viwanda nchini hivyo kuhusu changamoto ya upatikanaji wa changamoto ya makaa ya  mawe wataitua.


Awali,Mkurugenzi wa Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement,Reinhardt Swart,alimuambia Waziri Mkuu kuwa hivi karibuni kiwanda hicho kimekumbwa na changamoto ya nishati,usafirishaji ambapo uzalishaji ni mkubwa lakini usafirishaji ni mdogo kutokana sehemu kubwa wanatumia usafiri wa treni kusafirisha saruji lakini mabehewa yanayokuja ni kidogo ukilinganisha na uzalishaji kuwa mkubwa.


Amesema kuwa kiwanda hicho ni muhimu kwa uchumi wan chi na watu wa Tanga kutokana kimeajiri wafanyakazi 360 na kutoa ajira zisizo rasmi 600.
o kujiuzulu nafasi yake mwaka 2018.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: