Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema Serikali imekusudia kumnyanga’anya shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga kwa kusababisha migogoro kwa wakazi wa eneo hilo na kukiuka masharti ya uendelezaji.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo pamoja na wamiliki wa shamba hilo la Kwashemshi Sisal Estate mara baada ya kukagua miundombinu ya shamba hilo ambayo imeonekana kuchakaa.

“kwanza umekiuka masharti ya uendelezaji, kwa sababu umepewa shamba tangu mwaka 2003 na hadi leo ni miaka 17 hujalima lote wakati ulitakiwa uwe umemaliza kulilima mwaka 2011. Pili tunakudai kodi ya pango la ardhi hujalipa, tatu hujatoa ajira kwa wananchi na hujatoa gawio kwa Halmashauri, sasa kwanini nisimshawishi Mhe. Rais afute hili shamba?” amesema Mhe. Lukuvi.

Awali mkazi wa eneo hilo Bwana Musa Majaliwa amemlalamikia mwekezaji huyo kwa madai ya kumiliki shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari elfu tatu ambapo katika eneo lote ekari mia tatu pekee ndiyo zenye mkonge na sehemu nyingine ni vichaka.

“tunachoomba Waziri Lukuvi utusaidia kupata sehemu ya ardhi hii kwa matumizi ya kilimo na makazi kwa kuwa ongezeko la watu limekuwa ni kubwa tofauti na hapo awali” alisema Bwana Musa.

Kwa mujibu wa Mhe. Waziri shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 3,703 linamilikiwa na Ndugu Methew Upanga Mnkande maendelezo yake hayaridhishi kwani hadi sasa eneo lenye mkonge wakuvuna (Mature) ni ekari 1,210, eneo lenye mkonge mdogo (Immature) ni ekari 380 na kufanya eneo lililoendelezwa kuwa na ukubwa wa ekari 1,590 sawa na asilimia 42 tu.

Kuhusu kudaiwa kodi, mmiliki huyo tangu amilikishwe mwaka 2003 alikuwa hajalipa kodi ya pango la ardhi na alikuwa anadaiwa shilingi 2//6yyyy 2,218,000 ambapo hadi sasa amelipa shilingi 8, 000,00 na deni hadi sasa anadaiwa shilingi 14,218,000.

Kwa upande wake Mwakilishi wa mwekezaji wa shamba hilo ambae anatambulika kwa jina la mzee Mkande amedai kuwa shamba hilo limeendelezwa kwa kupanda mikonge mikubwa hekta mia nne thamani na mkonge mdogo ambao unatajiwa kuvnwa hivi karibuni ni hekta 150.

Kuhusu madai ya kodi ya pango la ardhi wanazodaiwa na Serikali mwakilishi huyo amekili kuwa awali walikuwa hawalipi kodi, ila sasa wameingia makubaliano na wilaya kulipa ambapo mpaka sasa wameshalipa kiasi cha shilingi milioni 8 na bado wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 14 mpaka sasa.

Hata hivyo, Mhe. Lukuvi aliendelea kumbana mwakilishi huyo kwa kumfahamisha kuwa shamba hili lipo kwenye hatua za ubatilishaji kutokana na uvunjifu wa masharti ya kutoendeleza ipasavyo na kulipa kodi ya ardhi kwa kusuasua.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wasimamizi wa shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga mbele ya wakazi wa eneo hilo. Kulia ni bwana John Mjengwa na katikati ni Mzee Mkande.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua miundombinu ya shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wasimamizi wa shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga mbele ya wakazi wa eneo hilo.

 Baadhi ya miundombinu chakavu ya shamba la mkonge la Kwashemshi Sisal Estate lililopo kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga.
Wakazi wa kata ya Kwashemshi wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
Share To:

Post A Comment: