Wednesday, 4 March 2020

RANCHI YA TAIFA KONGWA YAANZA KUTOA CHANJO


 
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kampuni ya Ranchi ya taifa- kongwa- imeanza kutoa chanjo kwa mifugo inayofugwa ndani ya hifadhi hiyo ili kukabiliana na magonjwa yanayopelekea vifo kwa mifugo.

Akizungumza katika zoezi hilo kaimu meneja wa kampuni ya ranchi za taifa masele shilagi amesema hadi kufikia leo zaidi ya ng'ombe elfu ishirini na nne na mia tisa tayari wamechanjwa ili kukinga na magonjwa na kuwa na mfungo bora anayekidhi soko la dunia
huku akitoa rai kwa wananchi kuwa na ushirikiano katika zoezi hilo.
Ngonyani uledi ni mwenyekiti wa umoja wa wafugaji wanaozunguka ranchi ya taifa kongwa amesema zoezi hilo linaendelea vizuri.
Afisa mifugo mwandamizi msaidizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi , idara ya Uzalishaji wa mifugo na Masoko CHARLES NGAMALA akimwakilisha mkurugenzi wa Idara hiyo amesema wizara ya Mifugo na Uvuvi ina mikakati mbalimbali katika kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya  mifugo unaongezeka


Daktari wa Mifugo katika Ranchi ya Kongwa,Noel Makawaja ambaye ndiye anaifanya kazi hiyo amesema kwa sasa chanjo inayo chanjwa ni ya ugonjwa wa upele ngozi ya ng'ombe ambapo ugonjwa huu ukitokea huharibu hata ubora wa ngozi na kusababisha ngozi  ziwe na daraja la chini lisilokuwa na bei ya kumpatia mfugaji  faida.


No comments:

Post a comment