Mkurugenzi  mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako ameweka jiwe la msingi katika awamu ya pili katika Tume hiyo iliyopo Mkoani Arusha
Dr.Remigius Kawala Mkurugenzi wa ufundi na huduma za Taasisi akimpa maelezo kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako namna ya kuandaa sampuli na kuchakata matokeo ya viasili vya mionzi kwenye mazingira,akipotembelea maabara na kukagua maendeleo ya ujenzi 
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akikagua  maendeleo ya ujenzi wa awamu ya pili wa  maabara changaman maabara 8 za kiuchunguzi na kituo cha  mafunzo ya usalama na kinga dhidi ya maradhi katika makao makuu ya Tume ya Ngauvu za Atomiki Tanzania iliyopo mkoani Arusha utakaogharimu shilingi Bilioni 10.4

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala mara baada ya kuweka jiwe la msingi na kukagua maendeleo ya ujenzi.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala,Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, mkuu wa Chuo cha Techical Arusha,Mkurugenzi mkuu wa Temdo,Makaku mkuu waChuo cha Nelson Mandela,Mkandarasi
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala,Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,Mkurugenzi mkuu wa Temdo,Makaku mkuu waChuo cha Nelson Mandela,Mkandarasi 
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala,Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,Mkurugenzi mkuu wa Temdo,Makaku mkuu waChuo cha Nelson Mandela,Mkandarasi pamoja na wafanyakazi wa ujenzi .
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala,Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,Mkurugenzi mkuu wa Temdo,Makaku mkuu waChuo cha Nelson Mandela,Mkandarasi pamoja na wafanyakazi wa ujenzi unaoendelea kutoka kampuni ya 
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala,Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi katika Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelezo kutoka kwa mkuu wa idara ya huduma ya kuhifadhi kinga ya mionzi Yesaya Sungita juu ya mahabara ya kuhakiki ubora wa vifaa na miundombinu ili kuangalia kama yametengenezwa katika ubora unaohitajika 


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako ameweka jiwe la msingi katika awamu ya pili ya ujenzi wa maabara 8 za kiuchunguzi na kituo cha  mafunzo ya usalama na kinga dhidi ya maradhi katika makao makuu ya Tume ya Ngauvu za Atomiki Tanzania iliyopo mkoani Arusha utakaogharimu shilingi Bilioni 10.4

Akizungumza katika hafla hiyo Prof.Ndalichako amesema kuwa maabara hiyo inajengwa ili kuhakikisha uendelezaji wa matumizi salama ya teknolojia hapa nchini ambapo katika ukanda wa Afrika nchi ya Tanzania itakuwa ya pili kuwa na mahabara kubwa ya kisasa.

Prof.Ndalichako amesema Serikali ya India kupitia ubalozi wake hapa nchini na Shirika la Nguvu za Atomiki duniani imewezesha upatikanaji wa mashine zenye thamani ya shilingi bilioni 2.4 ambazo zinalenga kuimarisha matumizi ya teknolojia ya nyuklia katika kutibu maradhi ya saratani katika hospitali ya ocean Road na  Bugando .

Kwa upande wake Mkurugenzi  mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Prof.Lazaro Busagala amesema kuwa serikali ilianzisha mradi wa kujenga mahabara Changamano katika makao makuu ya TAEC Arusha kwa lengo la kuiongezea uwezo wa usimamizi na uendelezaji wa matumizi salama ya nguvu za Atom nchini

Amesema maabara changamano ya awamu ya pili inakadiriwa kuwa na ukubwa wa mita mraba 10,500 ambapo kutakuwa na mahabara 8 kwa ujumla wake za kiuchunguzi na kituo cha mafunzo cha usalama na kinga dhidi ya madhara ya mionzi na itakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi,watafiti wa ndani na wanje ya nchi ambao wanakadiriwa kuwa wapatao 2200 kwa mwaka

Prof.Busagala  amesema ujenzi wa maabara hiyo utasaidia kuzalisha wataalam zaidi katika Nyanja ya teknolojia ya nyuklia ili kusaidia kukuza uchumi kupitia mchango katika teknolojia hiyo na itasaidia kuimarisha usalama wa mazingira na uchimbaji na usafirishaji wa madini ya uranium ambapo Tanzania inakadiriwa kuwa na ujazo wa tani 73,480

‘’Madini haya yapo sehemu mbalimbali kama vile
Namtumbo,Bahi,Galapo,Minjingu,Buru,Simanjiro,Like Natron Songea,Tunduru,Madaba Nachingwea,Chunya,Mbarali,Mbozi,Igunga,Iramba,Singida,Kondoa,Babati,Hanan’g,Handeni,Kilindi,Kongwa,Ngomero,Kilosa Chamwino,Mpwapwa,Kiteto,Bagamoyo na Korogwe.’’ alisema Prof.Busagala

Prof.Busagala ameainisha faida za kuwa na Maabara hiyo kuwa ni pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi na uratibu,uelewa na usalama wa mionzi, wataweza kutambulika kimataifa,kuimarisha ubora wa vipimo,pamoja na kufanya utafiti.

Pia kuboresha huduma za mahabara ili kulinda wananchi dhidi ya mazingira yasiyo salama ya teknolojia ya nyuklia na kuongeza wigo wa mafunzo kwa vitendo ikiwemo usalama wananchi katika mambo ya nyuklia  

Ujenzi wa mahabara awamu ya kwanza ulikamilika na kuzinduliwa waziri mkuu wa Tanzania Kassimu Majaliwa April 2019 ambapo serikali ilitoa shilingi bilioni 2.3 zilizowezesha kukamilisha ujenzi huo

Amesema maabara changamano ya awamu ya pili inakadiriwa kuwa na ukubwa wa mita mraba 10,500 ambapo kutakuwa na mahabara 8 kwa ujumla wake za kiuchunguzi na kituo cha mafunzo cha usalama na kinga dhidi ya madhara ya mionzi na itakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi,watafiti wa ndani na wanje ya nchi ambao wanakadiriwa kuwa wapatao 2200 kwa mwaka

Akitoa salam za mkoa, Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa serikali ya mkoa ipo tayari kushirikiana na Tume ya Nguvu ya Atomiki  ili kuhakikisha kuwa  mahabara hiyo ya kisasa nay a kwanza kwa Afrika ya Mashariki  kuhakikisha malengo yote yaliyokusudiwa yanatekelezeka 

Aidha Gambo  amesema kuwa mkoa  upo salama kwa kushirikia na Wizara ya afya na Shirika la Afya Duniani hakuna mgonjwa aliyeongezeka kwani yule mgonjwa aliyedaiwa kuwa na ugonjwa wa Corona anaendelea vizuri,pia amesema kuwa  dereva aliyempakiza vipimo vinaonyesha kuwa yupo vizuri hana maambukizi yeye pamoja na mtandao wake wote.

Pia ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwa makini katika nyumba za ibada wazingatie miongozo yote iliyotolewa na wataalam wa Afya kwamba wahakikishe kabla muumini hajaingia kwenye kanisa kuwe na namna ya kujikinga na  maambukizi ya vurusi vya ugonjwa huo wa Corona

Gambo alisema ni vizuri viongozi wa dini wakawaongoza na kuwasisitiza waumini wote kuzingatia masharti hayo kwa usalama wao ,kwa usalama wa mkoa na kwa  Taifa pia.

''Tunaamini kwa vile waumini ni watu wasikivu na wanaongozwa na Roho siyo miili naamini kwamba wataendelea kutoa maangalizo kuhusiana na changamoto hii kubwa''Alisema Gambo
  
MWISHO
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: