Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Imeelezwa kuwa eneo la Nyerere Square Jijini Dodoma limekuwa ni moja ya maeneo yanayovutia  watu wengi kutembelea kwa ajili ya kupumzikia pamoja na kutalii hivyo kuwa na fursa kubwa kwa  Vijana kujipatia ajira hususan kupiga picha za kumbukumbu .
Hayo yamesemwa   leo na vijana wanaofanya shughuli ya kupiga picha katika eneo hilo la Nyerere Square jijini Dodoma  ambapo wameiambia Msumba News   kuwa  wepesi wa watu kukutana katika eneo hilo imewafanya kwao iwe fursa ya kujipatia ajira ya kupiga picha huku wakiiasa jamii kuendelea kuwa na desturi ya kutunza mazingira katika eneo hilo.
“Eneo hili limekuwa fursa kubwa ambapo imetufanya sisi vijana wa jijini hapa kujipatia ajira hususan ya kupiga picha watu mbalimbali wanaokuja hapa”alisema mmoja wa vijana hao.
Aidha,kutokana ugonjwa wa virusi  vya Corona wapiga picha hao wamesema kuwa wamejihadhari katika shughuli zao za kila siku.
Edwin Maiko Mchiwa naye ni mmoja wa wapiga picha katika eneo la Nyerere Square ambapo amebainisha kuwa yeye huwa anatumia ubunifu wa kupiga gitaa ili kuvutia zaidi wateja wanaotaka kupiga picha  hususan wale wenye ndoto za uimbaji.
“Eneo wamekuwa watu wengi wanavutiwa kufika katika eneo hili hivyo kuja na gitaa katika eneo hili imenifanya nifanye ubunifu huo ili kuvutia watu wengi kwani asilimia kubwa wanapenda kupigwa picha wakiwa na gitaa “amesema Edwin.
Mwenyekiti wa wapiga picha katika eneo la Nyerere Square jijini Dodoma  David Elias amewataka wananchi wanaotembelea katika eneo hilo kuwa wastaarabu katika utunzaji wa Mazingira huku akishauri kuwekwa mabango ya Picha mbalimbali za utalii  pamoja na runinga za Utalii katika eneo hilo ili kuvutia zaidi raia wa kigeni na Watazania  kwa ujumla kutembelea hifadhi mbalimbali za kitalii nchini ikiwemo mbuga za wanyama.
“Niwaase Watanzania wanaoingia humu wawe Wastaarabu katika utunzaji wa Mandhari ya eneo hili la Nyerere Square pia ningependekeza katika eneo hili kuwekewa mabango  ya utalii kila upande pia kufungwa channel za Utalii zinazoonesha Mbuga mbalimbali za wanyama pamoja na hifadhi na makumbusho mbalimbali ya Taifa hali hii itasaidia watu wanaokuja hapa kuvutiwa zaidi na maeneo mengine makubwa ya utalii yaliyopo nchini”amesema .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: