Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Mkoa wa Dodoma unatarajia kuandaa kongamano la Wadau wa Elimu kuanzia
tarehe 21-22/Machi/2020.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Machi,6,2020 jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amesema lengo  la kongamano hilo ni  kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta
ya Elimu Mkoani Dodoma hali ambayo husababisha kiwango cha elimu kuwa
cha chini mkoani hapa licha ya kuwa ni makao makuu ya nchi.

Dkt.Mahenge ametaja baadhi ya viashiria vinavyosababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi katika mkoa wa Dodoma ni pamoja na umbali mrefu wa shule  ,ufuatiliaji hafifu pamoja na mwamko mdogo wa wazazi juu ya masuala ya elimu pamoja na miundombinu isiyokuwa toshelezi.

Hivyo kongamano hilo  litakutanisha wadau ili kuchambua mikakati
mbalimbali za kuinua kiwango cha elimu mkoani Dodoma ambapo kutakuwa
shughuli  kuu mbalimbali zikiwemo   kuzindua kampeni endelevu ya
ushiriki wa jamii katika uchangiaji wa ujenzi wa miundombinu ya shule
,kufanya tathmini ya hali ya maono ya wananchi ushiriki maendeleo ya
elimu ,kubainisha masuala ya kiupambele katika kuboresha sekta ya
elimu pamoja  kuamsha hamasa kwa jamii katika suala la elimu kwa kutoa
tuzo mbalimbali kwa  walioonesha juhudi  katika suala la elimu.

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Maria Limo amesema jamii inatakiwa kuelewa
dhana ya  sera ya elimu ya Msingi bila malipo kwani mzazi ana jukumu
la kumnunulia mtoto wake mahitaji ya Msingi ya shuleni.

Kaulimbiu katika kongamano hilo ni “kuinua Kiwango cha Elimu katika
Mkoa wa Dodoma huku Mgeni Rasmi anayetarajiwa katika Kongamano hilo ni
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa
Majaliwa .

Share To:

msumbanews

Post A Comment: